Maelfu
kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa
nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee
Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa
rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa
Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013,
alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National
Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na
utawala wa Makaburu.
Baada
ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais
wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela
alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia
kipindi cha pili.
Kiasi
cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo
iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na
majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo
iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.
Mbali
na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine
mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack
Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu
wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu
hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais
watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill
Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani
wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais
Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi
wenzake katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa
Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini
ya Union Buildings mjini Pretoria.
No comments:
Post a Comment