Saturday, February 16, 2013

Kipindi cha Marehemu Reeva kuoneshwa kwenye luninga

Kampuni moja ya televisheni ya Afrika Kusini inasema itasonga mbele na mpango wake wa kutangaza kipindi kinachomuonesha Reeva Steenkamp, mchumba wa mawanariadha mlemavu, Oscar Pistorious.
Teeva Steenkamp, aliyekuwa mchumba wa Pistorius
Msichana huyo alipigwa risasi na kuuwawa nyumbani mwa Bwana Pistorious siku ya Alkhamisi na mwanariadha huyo sasa ameshtakiwa kwa mauaji yake.
Alipouwawa Reeva Steenkamp alikuwa anakaribia umaarufu mkubwa.
Mrembo huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 alikuwa ashiriki kwenye kipindi cha Tropical Island of Treasure ambacho kingetayarishwa nchini Jamaica.
Katika hatua ambayo itaonekana na utata shirika la habari la SABC limeamua kuonesha kipindi kimoja tayari kimesharikodiwa, licha ya mauaji ya Reeva Steenkamp.
Mtayarishi wa kipindi alisema kipindi cha juma hili kitakuwa kumbu-kumbu ya Reeva Steenkamp.
Wakati huohuo mabango yaliyokuwa mabara-barani yanayomuonesha mchumbawake, Oscar Pistorius, yanabanduliwa.
Pistorius bado anazuwiliwa na polisi baada ya kuifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana litasikizwa Jumanne.

Monday, February 11, 2013

Hivi mapigano haya ya Wakritu na waislamu kuhusiana na machijio ni mpaka lini?


Majeruhi Abdalah Ibarihim akiwa amejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa mapnga kichwani na watu wanaodaiwa kuwa ni Wakristo

Huyu naye ni majeruhi aliyetambuliwa kwa jina la Steven Andrea (34) ambaye anadaia kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni waislamu,

Mchungaji aliyethibitishwa hadi sasa ni wa kanisa la PAGT aliyetambuliwa kwa jina la Mathayo Kachira(33),Mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Thursday, February 7, 2013

Watakiwa kuwajali wanamgambo wanaozuia magendo ya kahawa maeneo ya mipakani-Massawe



Na Theonestina Juma, Kagera
MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Fabian Massawe ameutaka uongozi wa Wilaya zote za mkoa Kagera kuhakikisha wanawawezesha wanamgambo wanaokuwa kwenye vizuizi vya mipakani ili kuthibiti magendo ya kahawa  yanayo likosesha Taifa mapato.
Kwa mujibu wa   Kanali Massawe Mgambo hao wanawekwa kwenye vizuizi kwa lengo kuzuia magendo ya kahawa  ambapo miaka ya nyuma waliweza kuokoa zaidi ya bilioni 1.9 wakati huo hawakuwezeshwa  kwa chochote unategemea.
“Hawa wanamgambo kipindi cha nyuma waliweza kuokoa kahawa yenye thamani y ash. bilioni 1.9  bila kuwezeshwa na kwa chochote kile hivi mnadhamani kuwa wataendelea kuzuia wakati wana njaa? Alihoji na kusema matokeo yake wataanza kupokea rushwa na kuruhusu kahawa ivushwe na kupelekwa nje ya nchi na kulikosesha Taifa mapato”alisema Massawe
 “Naagiza kama mnataka magendo ya kahawa iishe na tuweze kuongeza pato la Taifa tuhakikishe tunawalipa walinzi hao,tuwawezeshe kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani  kati ya bil. 1.9 walizookoa mkitoa milioni 40 mkawalipa mnapungukiwa nini ?alihoji  na kuongeza
“Ukitaka kupata pesa lazima utumie pesa ,ila mkiambiwa hivyo mnadai kuwa Wilaya na Halmashauri hazina pesa mbona mkiitwa kwenye vikao na Semina Dar es Salaam pesa ya kupanda ndege haikosi?kwa hiyo na hiyo itafutwe hatuwezi kukosa mapato hivi hivi mwaka jana kahawa nyingi imevushwa nje mwaka huu hatutaki kusikia ikivushwa “alisema.
 Katika hatua nyingine mkuu huyo aliwataka watendaji wote wa Serikali mkoania hapa kutochanganya kazi na Siasa badala yake wafanye kazi kwa kufuata viapo vyao walivyotoa wakati wakiomba kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
 Alisema kuwa Mkaguzi mkuuwa Serikalia anakuja mkoani humo anataka kukuta mambo yote yakiwa sawa kwa hiyo “Nawatahadharisha watendaji wanaorudisha nyuma maendelo kwa maksudi kwa kushindwa kumaliza miradi ya maendeleo wakati pesa nyingi yha Sarikali imetolewa kwa kisingizio ati sikitaki chama cha mapinduzi wasichang’anye kazi na siasa wachague moja.
 “Kuna watendaji wanatuhujumu kwa kurudisha nyuma maendeleo kwa sababu ya itikadi zao za vyama vya siasa hiyo ni dhambi hatuwatendei wananchi haki zao kwani wao ndio waajiri wetu tunapokea mishahara kutokana na kodi zao tuweke pembeni siasa tufanyekazi tuache malumbano penye vurugu za kidini au siasa hapawezi kuwa na amani wala maendeleo”alisema
 Asema kuwa tofauti za kisiasa kati ya watendaji na madiwani imekuwa ikisababisha miradi mingi kutokamilika kwa wakati na mingine kukwama kabisa kwa hiyo sheria ndogo zitumike kuwabana hao wasiojua kuwa maendeleo ni nguzo muhimu katika Taifa letu.
Mwisho


Thursday, January 31, 2013

10 Wahofiwa kufa maji Zanzibar


Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso 

Zanzibar
BOTI ya abiria iliyokuwa ikitokea Pangani mkoani Tanga kwenda Zanzibar ikiwa na watu 32 juzi usiku ilizama katika eneo la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Zanzibar ambapo watu 10 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha.

Taaarifa zilizofikia gazeti hili jana jioni zilisema kati ya abiria 27 na wafanyakazi watano waliokuwa kwenye boti hiyo, ni watu 20 tu waliokuwa wameokolewa wakati wengine 10 wakiwa hawajulikani walipo.

Msemaji wa Mkuu wa Polisi nchini, Advera Senso alisema jahazi liitwalo Sunrise liliondoka Tanga juzi saa 2:00 usiku kuelekea Zanzibar, lakini lilipigwa na dhoruba katika eneo la Nungwi.

“Mpaka sasa watu 22 wameokolewa akiwamo nahodha Abdallah Selemani, kumi wanatafutwa ijapokuwa wanahofiwa kuwa wameishakufa. Kati ya hao ni watoto watatu na watu wazima ni saba,”alisema Senso katika ujumbe alioutuma kupitia simu yake ya mkononi.

Aliendelea: “Boti kutoka Tanga ipo kwenye eneo la tukio kusaidia uokozi na wakazi wa Kaskazini Unguja wamepokea watu waliookolewa na kuwapa huduma. Taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia Tanga na Zanzibar”.

Hata hivyo idadi ya watu waliookolewa kwa mujibu wa Senso ilitofautiana na ile iliyokuwa imetolewa awali na Kamanda wa Wanamaji na Bandarini Zanzibar, SP Martin Lisu aliyesema juhudi za kuwaokoa abiria hao zilikuwa zikiendelea na kwamba waliokuwa wamepatikana wakiwa hai ni watu 21.

Lisu alisema abiria hao walionusurika kifo walipelekwa hospitalini kwa ajili ya kuchunguzwa afya zao na wengine walipatiwa huduma za kwanza kutokana na mshtuko walioupata.

“Kusema kweli tulifanikuwa kuwaokoa abiria 21 na wengine siwezi kusema kama wamezama ila nachoweza kusema ni kwamba bado hatujawapata,” alisema Kamanda Lisu na kuongeza:
“Taarifa nilizonazo ni kwamba, hii boti ilikuwa ikitokea Pangani, ilipofika eneo la Nungwi ikakubwa na dhoruba kali na kisha kuanza kupoteza mwelekeo”.

Eneo la Nungwi
Eneo la Nugwi lina historia ya kusababisha ajali za mara kwa mara na mara ya mwisho ndiko ilitokea ajali ya meli ya MV Spice Islander iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400 mwaka 2011.

Ajali hiyo ilielezwa kusababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji ikiwemo kukosekana kwa ukaguzi kabla ya meli hiyo kuondoka.Taarifa zilizema kuwa meli hiyo ilizidisha idadi ya abiria na mizigo hivyo ilipofika eneo la Nungwi ilizidiwa na kuanza kuzama.

Katika kujaribu kusaka ukweli wa mambo, Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein aliunda tume maalumu kuchunguza mazingira yaliyosababisha ajili hiyo.
Ripoti ya tume hiyo ilifichua uzembe uliojitokeza kwenye mamlaka husika na kupendekeza hatua kadhaa ili kuimarisha hali ya usafiri kwenye maji.

Ajali nyingine kubwa ni ya meli ya MV Skagit iliyotokea mwaka jana ikiwa inakaribia katika bandari ya Zanzibar, ambayo hatua za awali za uokoaji zilishindikana na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Ni kipindi kirefu hatujapata wala kumuona sangara mkubwa kiasi hiki

 Baadhi ya wafanyabishara wa soko kuu la Muleba mjini wakishangaa kumuona samaki aina ya sangara mwnye kilo zaidi ya 40 akiwa ameletwa sokoni humo kwa ajili ya kuuzwa.Mwenye samaki huyo,  Bw.Deocres John mwenye kofia kichwani alisema ni miaka mingi hajawahi kupata samaki kama huyo ambapo samaki huyo alikuwa akiuzwa sh. 100,000 baada ya kuondolewa bon do lake lililokuwa na uzito wa nusu kilo ambalo huuzwa sh. 40,000.

Tuwafundishe watoto wetu kufanya kazi za ndani



 Mtoto umuleavyo ndivyo akuaaji , hapa mtoto Rainer Jeremia miaka 5 akimsaidia mama yake kufuta vyombo baada ya kuviosha.

Wednesday, January 30, 2013

Lulu Karibu uraiani na uwe makini kwa kila jambo

 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililompeleka Mahakama Kuu kukamilisha taratibu za kupata dhamana.
Lulu akiingia Mahakamani
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyuma akifuatiwa na mama yake mzazi.
Lulu akiondoka mahakama hapo.

Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. 
Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kuwasilisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa Msajili wa Mahakama kila mwezi.