Na Theonestina Juma, Kagera
MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Fabian Massawe
ameutaka uongozi wa Wilaya zote za mkoa Kagera kuhakikisha wanawawezesha wanamgambo
wanaokuwa kwenye vizuizi vya mipakani ili kuthibiti magendo ya kahawa
yanayo likosesha Taifa mapato.
Kwa mujibu wa Kanali Massawe Mgambo
hao wanawekwa kwenye vizuizi kwa lengo kuzuia magendo ya kahawa ambapo miaka ya nyuma waliweza kuokoa zaidi ya
bilioni 1.9 wakati huo hawakuwezeshwa kwa chochote unategemea.
“Hawa wanamgambo kipindi cha nyuma waliweza
kuokoa kahawa yenye thamani y ash. bilioni 1.9 bila kuwezeshwa na kwa chochote kile hivi
mnadhamani kuwa wataendelea kuzuia wakati wana njaa? Alihoji na kusema matokeo
yake wataanza kupokea rushwa na kuruhusu kahawa ivushwe na kupelekwa nje ya
nchi na kulikosesha Taifa mapato”alisema Massawe
“Naagiza kama mnataka magendo ya kahawa
iishe na tuweze kuongeza pato la Taifa tuhakikishe tunawalipa walinzi
hao,tuwawezeshe kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani kati ya bil. 1.9
walizookoa mkitoa milioni 40 mkawalipa mnapungukiwa nini ?alihoji na kuongeza
“Ukitaka kupata pesa lazima utumie pesa ,ila
mkiambiwa hivyo mnadai kuwa Wilaya na Halmashauri hazina pesa mbona mkiitwa
kwenye vikao na Semina Dar es Salaam pesa ya kupanda ndege haikosi?kwa hiyo na
hiyo itafutwe hatuwezi kukosa mapato hivi hivi mwaka jana kahawa nyingi
imevushwa nje mwaka huu hatutaki kusikia ikivushwa “alisema.
Katika hatua nyingine mkuu huyo aliwataka
watendaji wote wa Serikali mkoania hapa kutochanganya kazi na Siasa badala yake
wafanye kazi kwa kufuata viapo vyao walivyotoa wakati wakiomba kazi ili
kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema kuwa Mkaguzi mkuuwa Serikalia anakuja
mkoani humo anataka kukuta mambo yote yakiwa sawa kwa hiyo “Nawatahadharisha
watendaji wanaorudisha nyuma maendelo kwa maksudi kwa kushindwa kumaliza miradi
ya maendeleo wakati pesa nyingi yha Sarikali imetolewa kwa kisingizio ati
sikitaki chama cha mapinduzi wasichang’anye kazi na siasa wachague moja.
“Kuna watendaji wanatuhujumu kwa kurudisha
nyuma maendeleo kwa sababu ya itikadi zao za vyama vya siasa hiyo ni dhambi
hatuwatendei wananchi haki zao kwani wao ndio waajiri wetu tunapokea mishahara
kutokana na kodi zao tuweke pembeni siasa tufanyekazi tuache malumbano penye
vurugu za kidini au siasa hapawezi kuwa na amani wala maendeleo”alisema
Asema kuwa tofauti za kisiasa kati ya
watendaji na madiwani imekuwa ikisababisha miradi mingi kutokamilika kwa wakati
na mingine kukwama kabisa kwa hiyo sheria ndogo zitumike kuwabana hao wasiojua
kuwa maendeleo ni nguzo muhimu katika Taifa letu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment