Saturday, February 16, 2013

Kipindi cha Marehemu Reeva kuoneshwa kwenye luninga

Kampuni moja ya televisheni ya Afrika Kusini inasema itasonga mbele na mpango wake wa kutangaza kipindi kinachomuonesha Reeva Steenkamp, mchumba wa mawanariadha mlemavu, Oscar Pistorious.
Teeva Steenkamp, aliyekuwa mchumba wa Pistorius
Msichana huyo alipigwa risasi na kuuwawa nyumbani mwa Bwana Pistorious siku ya Alkhamisi na mwanariadha huyo sasa ameshtakiwa kwa mauaji yake.
Alipouwawa Reeva Steenkamp alikuwa anakaribia umaarufu mkubwa.
Mrembo huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 alikuwa ashiriki kwenye kipindi cha Tropical Island of Treasure ambacho kingetayarishwa nchini Jamaica.
Katika hatua ambayo itaonekana na utata shirika la habari la SABC limeamua kuonesha kipindi kimoja tayari kimesharikodiwa, licha ya mauaji ya Reeva Steenkamp.
Mtayarishi wa kipindi alisema kipindi cha juma hili kitakuwa kumbu-kumbu ya Reeva Steenkamp.
Wakati huohuo mabango yaliyokuwa mabara-barani yanayomuonesha mchumbawake, Oscar Pistorius, yanabanduliwa.
Pistorius bado anazuwiliwa na polisi baada ya kuifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana litasikizwa Jumanne.

No comments:

Post a Comment