Wednesday, August 14, 2013

Tunapata wakati mugumu kupata ukweli wa Diwani wa CCm kutekwa,anakosema alikwenda ni miezi mitano hajawahi kukanyaga

Na Theonestina  Juma, Kagera
  JESHI la polisi mkoani Kagera  linapata wakati mugumu wa kupata ukweli wa mazingira ya utekwaji wa diwani wa ( CCM ) Bw.Arnold Rwesheleka, kata ya Chonyonyo Wilayani Karagwe, na  watu wanaosadikika kuwa ni majambazi na kisha gari lake kulitekekeza kwa moto katika pori la kimisi.
 Akiongea  na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera  Philip Kalangi  alisema mazingira ya utekwaji wa diwani  huyo pamoja na maelezo yake  yanatia mashaka.
 Alisema  maelezo ya mlalamikaji yanajichanganya  hali hiyo imesababisha jeshi hilo kuwa na mashaka ya mazingira ya kutekwa  kwa diwani  huyo (CCM) alitekwa na watu watatu wasiojulikana wakiwa na bunduki aina ya piston ila alifanikiwa kutoroka kabla ya kudhuruwa.
  Alisema jeshi la polisi liliopofika  eneo la tukio mazingira yalionyesha kulikuwa na maandalizi ya  kuchomwa kwa gari hilo na huko alikodai kuwa ,alienda kusalimia na alikuwa hajaenda huko takribani miezi mitano.
 “Tulishazoea kukagua maeneo mengi yanayokuwa yamefanyiwa uhalifu na matukio mbalimbali lakini mazingira, aliyoteketezwa gari lake yana utata”alisema kamanda Kalangi.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kina  na tayari kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa ( RCO ) Bw.Henry Mwaibambe yuko Karagwe kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
 Alisema  kutokana na utata wa mzingira ya utekwaji huo  wanatafuta kumbukumbu mbalimbali za mlalamikaji zikiwemo za gari pamoja na bima ya gari  kuangalia kama kulikuwa na matatizo kabla ya gari hilo kuteketezwa na moto.

Na Theonestina Juma

Awali  diwani huyo alidai katika kituo cha polisi kuwa alitekwa na watu watatu wasiojulikana wakiwa na bunduki aina ya piston ila alifanikiwa kutoroka kabla  hawajamdhuru baada ya kuwatoroka kwa kuwafungia ndani ya gari lake na kwa hasira wakateketeza gari lake kwa moto.

Alisema  Bw. Rwesheleka alipita katika kizuizi cha polisi cha Chanyamisa majira ya saa 11.jioni akisema kuwa anaelekea katika kijiji cha Nyakasimbi kumuona bibi yake ambaye alidai kuwa ni mgonjwa.

Alisema kuwa majira ya saa mbili za usiku ambapo diwani akiwa safarini kurudi Chonyonyo alikutana na mtu mmoja ambaye alimsimamisha na kisha kumtisha kwa kumuonyesha silaha,  akamwamuru diwani huyo kugeuza gari na kurudi  barabara ya Benako ambapo diwani huyo alilazimika kufuata maagizo hayo.

Alisema wakati diwani akiendelea na safari kuelekea aliko elekezwa mbele kidogo walikutana na watu wengine wawili ambapo huyo mwenye silaha aliyekuwa ndani ya gari alimwamuru asimamishe gari ndipo watu hao walianza  kupakiza mizigo ndani ya gari.

Alisema kutokana na maelezo ya diwani huyo kuwa wakati watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiendelea kupakiza mizigo ndani ya gari, diwani alifanikiwa kutoroka na kutokomea porini ambapo alikimbia  kisha akifanikiwa kuingia katika barabara iendayo Karagwe ndipo  ghafla likatokea gari aina ya Hiace lililokuwa likitokea Benako kwenda karagwe na kumpa msaada.

Alisema kuwa wakati diwani huyo akiwa ndani ya Hiace aliambiwa na wasafiri kuwa wameona gari lake likiwaka moto  katika maeneo ya Nyakasimbi ambapo majira ya saa 3.30 usiku Bw.Rwesheleka alifika katika kituo kidogo cha polisi Chanyamisa na kutoa taarifa kuwa katekwa na majambazi.

Alisema baada ya kutoa taarifa polisi waliondoka na diwani huyo mpaka eneo la tukio na kukuta gari hilo likiendelea kuteketea kwa moto,kamanda aliongeza kuwa polisi wanaendeleana uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo kwani mazingira yake yanatatanisha na wataendelea kutoa taarifa zaidi pindi watakapo wakamata wahusika.
tika maeneo ya Nyakasimbi ambapo majira ya saa 3.30 usiku Bw.Rwesheleka alifika katika kituo kidogo cha polisi Chanyamisa na kutoa taarifa kuwa katekwa na majambazi.

 Alisema baada ya kutoa taarifa polisi waliondoka na diwani huyo mpaka eneo la tukio na kukuta gari hilo likiendelea kuteketea kwa moto,kamanda aliongeza kuwa polisi wanaendeleana uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo kwani mazingira yake yanatatanisha na wataendelea kutoa taarifa zaidi pindi watakapo wakamata wahusika.

Tuesday, August 13, 2013

CCM Kagera watimuwa madiwani wake wanane kwa kukihujumu

Na Theonestina Juma

HALMASHAURI kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Kagera,imewafukuza  madiwani wake  nane katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa kile kilichoelezwa kuwa ni  kupuuza ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM taifa  Rais  Jakaya Kikwete.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa niaba ya halmashauri kuu ya CCM mkoa, Katibu Mkuu wa chama hicho mkoa wa Kagera, Bw. Avelin Mushi,alisema kuwa uhamuzi huo umekuja kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.

Mushi amewataja madiwani hao nane kuwa  ni pamoja na Bw.Yusuph Ngaiza,kata Kashai ambaye pia ni Mwenyekiti wa ccm wilaya Bukoba, Bw.Samwel Ruangisa(Kitendaguro) meya mstaafu na mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera.

Wengine ni  Bi.Murungi Kichwabuta(Viti maalumu) Bw.Deusdedith Mutakyawa(Nyanga) Bw.Richard Gaspar(Miembeni), Bw.Alexander Ngalinda(Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu meya  Bw.Dauda Kalumuna(Ijuganyondo)na  Bw.Robert Katunzi wa kata Hamugembe.

Bw.Mushi alisema  kuwa  kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambavyo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kupatakana kwani hakuna vita visivyokuwa na mwisho wake.

Pia, alisema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.

Wahamiaji haramu 7814 waondoka Kagera, Wanyarwanda 166 watimkia Uganda na mifugo yao

Na Theonestina Juma

JUMLA ya wahamiaji haramu 7814 waliokuwa wakiishi mkoani  Kagera  wameripotiwa kuondoka nchini kupitia mipaka zaidi ya  10 zilizoko mkoani hapa kufuatia agizo  la Rais Jakaya Kikwete  la kuwataka kuondoka ndani ya siku 14 alizotoa kwao.

  Akizungumza na Mwandishi habari wa gazeti  hili ofisini kwake jana , Naibu Kamishna wa uhamiaji ambaye ni Kaimu afisa uhamiaji Mkoa  wa Kagera,Bw. Elizeus Mushongi alisema idadi hiyo ya wahamiaji haramu walioripoti katika vituo mbalimbali vya uhamiaji vilivyopo mkoani hapa ni ndogo ikilinganishwa na wahamiaji wanaondoka kupitia njia za panya ambao ni wengi.

 Aliswema kituo kinachoongoza kupitisha wahamiaji haramu wengi ni cha Rusumo  ambacho kimewapitisha jumla ya wahamiaji  haramu 4748 wakielekea nchini Rwanda.

 Mushongi alisema katika makundi hayo ya wahamiaji haramu ambao wanatoka katika nchi tatu ambazo ni Uganda,Burundi na Rwanda kuna wahamiaji wengine ambao hawataki kururudi kwao na idadi kubwa ya wasiotaka kurudi kwao ni Wanyarwanda  wanaojiorodhesha katika vituo wakielekea Burundi na Uganda.

 Halikadhalika wengi wao wameeonekana wakipita njia za panya wakielekea nchi hizo pia.

 Alisema  katika  vituo  vya  Murusagamba walipita wanayarwanda 35 wakielekea Burundi,Mutukula 13 wakielekea Uganda,Bugango 22wakielekea Uganda,Kanyigo saba wakielekea Uganda.

 Halikadhalika kituo cha Kabanga Warundi  522  wamepita kurudi nchini mwao na 10 kupitia kituo cha Murongo kuelekea Uganda katika kituo hicho Wanyarwanda 166 walipitia hapo kuelekea nchini Uganda.

  Alisema kituo cha Murongo kimepitisha jumla ya wahamiaji 332,Murusagamba 78 na Mutukula 31 na eneo la Mgoma ambalo hakuna vituo vya idara ya uhamiaji walijisalimisha wahamiaji haramu 1734  katika ofisi za vijiji.

 Alisema  idadi ya ng’ombe walioondoka hadi kufikia jana walioripotiwa ni 1996 kupitia kituo cha Rusumo hata hivyo alisema kuwa ng’ombe wengi wanaelekea Uganda  kwa sababu Rwanda hawataki idadi kubwa ya Ng’ombe.

 Alisema kwa mujibu wa takwimu za wahamaiji haramu  walioondoka kwa hiari Wanyarwanda asilimia 64,warundi asilimia 34 na waganda,asilimia mbili.

 Alisema msako maalum haujaanza na unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa  na wameishaanza maandalizi.

 Hata hivyo aliwataka wahamiaji hao haramu waendelee kuondoka kwa hiari kabla hwajafikishwa kwenye mkono wa sharia.

 Aidha  alisema Idara ya uhamiaji Mkoa wa Kagera imesitisha utoaji wa vibali kwa muda wakisubiri maelekezo kutoka juu.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian  Massawe  amewatahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa msako huo wa wahamiaji haramu sambamba na kuwafichua waliojificha.

 Massawe  alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa  sheria  watu watakaobainika wakiwa ficha na kuwawekea vifua  wahamaiji haramu.

 Alisema msako huo utaanza muda wowote kuanzia sasa  na hawezi kutaja  siku rasmi  kwa sababu za kiusalama.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera  Philip  Kalangi alisema jumla ya silaha 42 zimewasilishwa kwa hiari na wahamiaji haramu kufuatia agizo la Rais lililoisha jana kutoka sehemu mbalimbali hapa Mkoani nyingi zikiwa ni magobore.

 Alisema  wahamiaji haramu wote watakaokamatwa  watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia.

Mwisho.