Na Theonestina Juma, Ngara
MWENYEKITI wa kijiji cha Kumwendo kata Mbuba Wilayani Ngara, Bw.Paul Rutishobwa (45) amehukumiwa kifungo cha maishajela na Mahakama ya Wilaya ya Ngara baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minane.
Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ngara,Bi.Mariam Lusewa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Awali mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi wilayani Ngara, Tumaini Membi aliiambia mahakama hiyo kuwa, Mwenyekiti huyo alitenda kosa hilo, Septemba 18, 2012 saa 2 usiku kijijini hapo.
Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa huyo alimwita mtoto huyo akiwa nyumbani kwao kwa lengo la kumtuma, ndipo alipomkamata na kumziba mdomo na kumvutia kwenye shamba la mihogo na kuanza kumbaka.
Alisema mtuhumiwa huyo alimvuta mtoto huyo umbali wa mita kama 15 kutoka nyumbani kwao ulikuwa na shamba la mihogo na kuanza kubaka.
Alisema mama wa mtoto huyo, Bi.Pelagia Gwassa
kwa wakati huo alikuwa akipika jikoni na alipomaliza shughuli za
mapishi ndipo alianza kumtafuta mwanae aje ale bila mafanikio, ndipo alipiga makelele kuwaita majirani ili wamsaidie kumtafuta
mwanae.
Alisema baadhi ya wananchi walijikusanya kuanza kumtafuta, ambapo walipofika kwenye shamba hilo la mihogo walisikia sauti ya mtoto huyo akisika kama anagugumia kwa maumivu.
Alisema walipomkaribia walimkuta akiwa anachuruzika damu kutoka sehemu zake siri huku akiwa amefungwa mdomo kwa kitambaa.
Alisema alipoulizwa amekuaje, alimtaja Bw.Rutishobwa kumvua nguo na kumwingilia na kisha kumwacha hapo.
Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Mabawe na kubaini kuwa amebakwa na kufikishwa mahakamani ambapo kipindi hicho chote alikuwa nje kwa mdhamana.
Hata hivyo, kwa upande wa mtuhumiwa akijitetea alidai kuwa hakumbaka mtoto huyo bali anasingiziwa.
Bw.Rutishobwa aliwaacha hoi mahakama hiyo baada ya kuhukumiwa maisha kwa kutoa hirizi mbili katika mkono wake wa kulia na kushoto na kuzitupa chini akidai kuwa mganga alimdanganya kuwa hatafungwa.
Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa Bw. Rutishobwa, aliwahi kuoa dada yake baba yake mtoto aliyebakwa, na kuzaa nae watoto wanne,na baadaye kutengana na hivyo mtoto aliyembaka alimzoea kwa sabbau ya undugu huo.
Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Tuesday, December 31, 2013
Kanisa Katoliki Ngara latishia kusitisha kuwabatiza watoto wa kiume
Na Theonestina Juma, Ngara
UONGOZI wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Ngara Mjini umetishia waumini wake kusitisha kuwabatiza watoto wao wa kiume wasipobadilika katika kuwabagua watoto wao katika kuwajenga kiimani.
Tishio hilo limetolewa jana na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Fransisco wa Asizi Parokia ya Ngara Mjini, Ivus Tindyebwa wakati akihubiri kanisani hapo ikiwa ni siku ya familia ilioenda sanjari na ubatizo wa watoto zaidi ya 40.
Kwa jinsi hali ilivyo katika malezi ya watoto,wazazi wengi wamekuwa wakiwalea watoto wao kimfumo dume, watoto wa kike wakiwa ndiyo wanawajibishwa zaidi huku watoto wa kiume wakiwa hawahimizwi hata kidogo kujishughulisha na masuala ya dini.
Hatua ya Paroko huyo kusema hayo ni kutokana Jumamosi Desemba 28, mwaka huu jimbo la Rulenge liliadhimisha siku ya utoto Mtakatifu,
wilayani Biharamulo na cha kushangaza watoto wa kike ndiyo walikuwa wengi kana kwamba siku hiyo ilikuwa ni utoto wa usichana."
"Itafikia hatua sasa siku ya utoto mtakatifu tutabadili iwe siku ya usichana mtakatifu, kwa sababu siku hiyo inayowalenga watoto wa jinsi zote na si watoto wa kike pekee"alisema Paroko huyo.
Aidha alihoji sababu ya waumini wa kanisa hilo kuegemea kwa watoto wa kike pekee na kuendelea kutoa malezi ya kiroho kiubaguzi uliojaa mfumo dume?
Hata hivyo alisema tatizo la kutoa malezi ya kiroho kiubaguzi haliko wa Jimbo la Runge tu bali ni tatizo kwa nchi nzima na hivyo ni wajibu wa waumini wa kanisa hilo kubadilka katika malezi ya watoto wao kiroho.
Alisema "wakristo wanatakiwa kubadili mfumo wa ulezi wa watoto wao kiroho kwa kuwahusisha watoto wa jinsi nzote".
Alisema licha ya wakati wa ubatizo hata majina ya watoto wa kiume yanakuwepo lakini anashangaa ikifika wakati wa huduma kanisani watoto wa kiume hawajitokezi na badala yake watoto wa kike ndiyo wanaonekana wengi.
Katika hatua nyingine Paroko huyo aliwakata vijana wa kanisa hilo kuachana na ndoa za kuwavuta kwa nguvu wasichana kwani inawafanya kuingia katika sakramenti hiyo bila kuchunguzana, kama wamekomaa kiakili na kimwili katika kulea familia yao kiroho.
Alisema wale wanaoingia katika ndoa kwa mfumo huo mwishoe ndoa yao inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutengana baada ya kujigundua kuwa hawawezi kuishi pamoja, jambo ambalo ni changamoto kwa kanisa.
UONGOZI wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Ngara Mjini umetishia waumini wake kusitisha kuwabatiza watoto wao wa kiume wasipobadilika katika kuwabagua watoto wao katika kuwajenga kiimani.
Tishio hilo limetolewa jana na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Fransisco wa Asizi Parokia ya Ngara Mjini, Ivus Tindyebwa wakati akihubiri kanisani hapo ikiwa ni siku ya familia ilioenda sanjari na ubatizo wa watoto zaidi ya 40.
Kwa jinsi hali ilivyo katika malezi ya watoto,wazazi wengi wamekuwa wakiwalea watoto wao kimfumo dume, watoto wa kike wakiwa ndiyo wanawajibishwa zaidi huku watoto wa kiume wakiwa hawahimizwi hata kidogo kujishughulisha na masuala ya dini.
Hatua ya Paroko huyo kusema hayo ni kutokana Jumamosi Desemba 28, mwaka huu jimbo la Rulenge liliadhimisha siku ya utoto Mtakatifu,
wilayani Biharamulo na cha kushangaza watoto wa kike ndiyo walikuwa wengi kana kwamba siku hiyo ilikuwa ni utoto wa usichana."
"Itafikia hatua sasa siku ya utoto mtakatifu tutabadili iwe siku ya usichana mtakatifu, kwa sababu siku hiyo inayowalenga watoto wa jinsi zote na si watoto wa kike pekee"alisema Paroko huyo.
Aidha alihoji sababu ya waumini wa kanisa hilo kuegemea kwa watoto wa kike pekee na kuendelea kutoa malezi ya kiroho kiubaguzi uliojaa mfumo dume?
Hata hivyo alisema tatizo la kutoa malezi ya kiroho kiubaguzi haliko wa Jimbo la Runge tu bali ni tatizo kwa nchi nzima na hivyo ni wajibu wa waumini wa kanisa hilo kubadilka katika malezi ya watoto wao kiroho.
Alisema "wakristo wanatakiwa kubadili mfumo wa ulezi wa watoto wao kiroho kwa kuwahusisha watoto wa jinsi nzote".
Alisema licha ya wakati wa ubatizo hata majina ya watoto wa kiume yanakuwepo lakini anashangaa ikifika wakati wa huduma kanisani watoto wa kiume hawajitokezi na badala yake watoto wa kike ndiyo wanaonekana wengi.
Katika hatua nyingine Paroko huyo aliwakata vijana wa kanisa hilo kuachana na ndoa za kuwavuta kwa nguvu wasichana kwani inawafanya kuingia katika sakramenti hiyo bila kuchunguzana, kama wamekomaa kiakili na kimwili katika kulea familia yao kiroho.
Alisema wale wanaoingia katika ndoa kwa mfumo huo mwishoe ndoa yao inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutengana baada ya kujigundua kuwa hawawezi kuishi pamoja, jambo ambalo ni changamoto kwa kanisa.
Monday, December 23, 2013
Wahamiaji haramu waliorejeshwa makwao na Operesheni kimbunga warudi Kagera, watishia wananchi,wawapora mali, wajiita M23
Na Theonestina Juma, Kagera
KATIKA hali
isiyo ya kawaida wahamiaji haramu waliorejeshwa nchini mwao na serikali ya
Tanzania kwa operesheni kimbunga
wamerejea kwa uwingi wilayani Kyerwa na kuwatishia wananchi kwa kujiita M23 na
kuwapora mali zao kwa nguvu.
Hayo
yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa, Mhandisi Benedict Kitenga wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera kanali, Massawe aliyembelea wilayani hapo kukagua maendeleo pamoja na ujenzi wa mabara
ya shule za sekondari za kata.
Alisema
kutokana kurejea kwa kasi ya ya ajabu kwa wahamiaji haramu katika kijiji na kata
ya Kibingo na kuwatishia wananchi wa kijiji
hicho kwa kujiita M23 kunawatia hofu wananchi hao.
“Wahamiaji
hao walikuwa wametengeneza makambi na kujihami kwa mapanga na marungu pia
walikuwa wakipita katika kijiji hicho na kuwatishia wananchi na
kuwanyanganya chakula kwa nguvu pia
kuwatishia maisha yao”alisema.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya kupata taarifa hizo walikwenda katika eneo hilo na kufanya operesheni
kubwa na kuwakamata wahamiaji haramu zaidi ya 20 pamoja na baadhi ya Watanzaia ambao walikuwa
wakishirikiana na wahamiaji haramu hao kuwahifadhi.
Alisema
Wahamiaji haramu hao waliokamtwa walirejeshwa kwenye nchi zao bila kutaja uraia
wao na watanzania walihusika walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Kutokana
na hali hiyo, alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa mara wawaonapo hao
wahamiaji haramu wakirejea au katika maeneo yao
Hata
hivyo, kwa upande wa Mkuu wa mkoa Kagera, kanali Fab ian Massawe alisema katika
operesheni Kimbunga waliondolewa wahamiaji haramu 31,000 badala ya 52,000 kwa hiyo
operesheni hiyo inaendelea ili kuhakikisha waliobaki wanaondolewa na hakuna wa
kurudi nchini.
“Chini
ya Kaulimbiu ya Hakuna wa Kubaki na
Hakuna wa Kurudi, tutahakikisha kila mhamiaji haramu anaondoka na watanzania
watakogundulika kushirikiana nao watachukuliwa hatua kali za kisheria, pia
naagiza Kamatia za Ulinzia na Usalaama kundelea na operesheni hiyo mpaka
kuwamaliza wahamiaji haramu.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa.
Mkuu
wa mkoa alisema ili kushughulikia tatizo hilo kikamilifu wananchi wanatakiwa
kutoa taarifa hasa kwa viongozi wa juu mfano kwake na mkuu wa wilaya ambapo
alitoa namba za simu zake kwa wananchi pamoja na mkuu wa wilaya ili kupambana
na tatizo hilo.
Hata
hivyo, baadhi ya wananchi waliohojiwa walisema tatizo la wahamiaji haramu
linasababishwa na baadhi ya watendaji wa serikali katika ngazi za chini ambao
wanachukua hongo na kuwarudisha katika mazingira ya wananchi.
Wananchi
hao walisema inavyoonekana, viongozi wa chini kuanzia ngazi ya vitongoji,
vijiji hadi kata wamepewa mamnlaka makubwa mno na pia wamekuwa wakikaa muda
mrefu bila kubadilishwa vituo vya kazi na hivyo kujenga mazoea na wahamiaji
haramu hao.
“Kinachoitakiwa
kifanyike ni serikali kuanzia ngazi ya wilaya kuanza tabia ya kuwatembelea
viongozi wa serikali za vitongoji hadi kata kwa kushtukiza ili kuweza
kutokomeza hii tabia iliojengeka mikongoni mwao na kuonekana kama miungu watu katika
maeneo yetu’alisema mwananchi mmoja.
Operesheni
kimbunga iliendeshwa hivi karibuni na serikali kwa kushirikisha vyombo mbali mbali vya usalama baada ya Rais Kikwete
kutoa wiki mbili kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini.
Friday, December 20, 2013
Waziri Kaghasheki atangaza kujiuzulu, mawaziri wengine watatu nao wafutwa kazi na Rais Kikwete
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imebainisha kuwa oparesheni Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa na Serikali ilikumbwa na unyanyasaji mkubwa wa wananchi, Ukatili, Udharirishaji, Ubakaji na Mauaji huku baadhi ya wazazi wakivuliwa nguo, kuteswa na kubakwa mbele ya wanafamilia.
Akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo Mwenyekiti wake James Lembeli amesema pamoja na mateso hayo yaliyowakumba wananchi pia nyumba zao zilichomwa na mifugo kupigwa risasi huku mingine ikifa kwa kukosa maji, chakula na maziwa kwa ndama wadogo.
Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa vitendo vya Rushwa vilivyotawala oparesheni Tokomeza ambapo pia wananchi waliokuwa na mifugo walitozwa faini na mifugo mingine kuuzwa kwa bei nafuu ambayo haikulingana na faini iliyokuwa ikitoza na wafugaji walizuiwa kushiriki mnada wa uuzaji wa mifugo hiyo.
Mbali na Waziri Kaghasheki mawaziri wengine watatu walioonekana kuwa wagumu kutamka na vinywa vyao kuwa wanajiuzulu, wamefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete katika taarifa yake iliotolewa mbungeni humo leo na Waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya kuwasiliana na naye akiwa nchini Marekani na kumwelezea Rais yote yanayojiri humo mjengoni.
WWaziri wa Emmanuel Nchimbi aliyewajibishwa na Rais Kikwete
Waziri wa Uvuvi na mifugo, Dkt. David Mathayo |
Waziri wa Shamsa Vuai Nahodha |
Tuesday, December 17, 2013
Kijijini Qunu kwao Nelson Mandela kulivyo
Qunu
ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini,
kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya
Butterworth na Mthata.
Kijiji
cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani na mahali ambapo Mzee
Nelson Mandela alizaliwa. Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri
ya kurejea.
Kijiji
cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa
Mvezo. Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela
amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa
utotoni.
Jumapili
ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi
ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. Alizikwa kwa heshima zote za
kiongozi wa Taifa katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya
milele.
Daraja la waendao kwa miguu likipita juu ya barabara mpya ya lami inayojengwa kuelekea kijijini Qunu.
Siku ya mazishi barabara ya kuelekea Qunu ilifungwa na ni magari yaliyokuwa na kibali tu ndiyo yaliyoruhusiwa kupita
Ulinzi ulikuwa mkali kila sehemu kijijini Qunu
Wageni wakiwa katika geti kuu la nyumba ya Mzee Mandela hapo Qunu
Nyumba ya Mzee Mandela
Nyumbani kwa Madiba kijijini Qunu
Hema maalumu zilikofanyika shuguli zote za mazishi. Kaburi lake liko nje ya hema upande wa kushoto
Hali ilivyokuwa saa kumi na moja alfajiri siku ya Jumapili
Nyumbani kwa Madiba kumejaa magari hata kabla ya jua kupanda angani
Sehemu ya kijiji cha Qunu. Mahema mbele ya nyumba ni ya wanahabari wa kimataifa waliopiga kambi hapo
Mandhari ya Qunu
Mandhari ya Qunu
Ni kijiji chenye mandhari nzuri. Wakati wa majira ya baridi barafu huanguka hapa
Qunu
Kila engo Qunu inapendeza
Kijiji cha Qunu
Bango linalotangaza kijiji cha Qunu kuwa cha urithi
Ulinzi ulikuwa si wa kawaida siku ya mazishi
Foleni ilikuwa ya kufa mtu
Wana Afrika Kusini toka kila kona walitembea umbali mrefu kwa miguu kuhudhuria mazishi
Nyimbo na ngoma vilitawala
Mdau akilipoza koo baada ya kutembea kwa muda mrefu
Sehemu ya mji wa Mthatha, kilomita kama 32 kutoka Qunu
Magari yalizuiwa kwa muda wakati mwili wa Mzee Madiba uliopowasili uwanja wa Mthatha na kupelekwa Qunu
Sehemu ya foleni ya magari ikikaribia mji wa Mthatha na hapa wakisubiri msafara wa mwili wa Mzee Mandela upite
Wednesday, December 11, 2013
Historia ya Rais Mandela yalivyoapanda na kushuka
Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mwafrika mweusi wa
Afrika Kusini,baada ya vita vya muda mrefu dhidi ya utawala wa kizungu.
Alizaliwa mkoani Eastern Cape, lakini baadaye akatorokea mjini
Johannesburg ambako alifanikiwa kuwa mwakili na kujiunga na haratakati
za chama cha ANC dhidi ya utawala wa kizungu.
Kama kijana, Mandela alipenda masumbwi. ''Masumbwi ni bure, Ukiwa
ulingoni , umri na hadhi yako pamoja na mali yako sio muhumu,''
aliandika katika kitabu chake kuhusu maisha yake
Mwaka 1956, alituhumiwa kwa kosa la uhaini kwa sababu ya kazi yake na
ANC. Wakati wa kesi yake, alikutana na mfanyakazi wa kijamii aliyeitwa,
Winnie Mandela. Ndao yake kwa Evelyn Mase iliisha baada ya wawili hao
kutalakiana.
Nelson na Winnie walioana mwaka 1958 lakini hawakufurahia maisha yao ya ndoa kwani wote walikuwa wakikamatwa mara kwa mara.
Kufuatia kesi ya pili ya uhaini dhidi ya Mandela, alifungwa maisha jela mwaka 1964
Hatimaye zaidi ya miaka ishirini baada ya kufungwa jela, Mandela aliachiliwa mwaka 1990.
Kufuatia kuachiliwa kwake, Mandela lizuru nchi nyingi na kukutana na
viongozi wa dunia alipokuwa anjiandaa kuwania urais. Anaonekana hapa
katika ubalozi wa Afrika Kusini mjini London ambako maandamano ya
kupinga utawala wa kizungu daima yalikuwa yakifanyika.
Mashauriano makubwa yalifanyika kabla ya rais FW de Klerk kukubali au
kuruhusu watu kupiga kura. Wawili hao walituzwa tuzo ya amani ya Nobbel,
kwa sababu ya kumaliza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Uchaguzi wa kwanaza wa kidemokrasia ulifanyika tarehe 27 mwezi Aprili
m,waka 1994. Waafrika weusi walipanga foleni kupiga kura kwa mara ya
kwanza. Chama cha ANC kilishinda uchaguzi huo kwa wingi wa kura na hivyo
Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi kuongoza Afrika Kusini
Mandela alitawala nchi hiyo kwa muhula mmoja pekee na mnamo mwaka 1999
akawa mmoja wa viongiozi wachache wa Afrika kuachia ngazi kwa hiari.
Thabo Mbeki, alipewa jukumu la kumrithi Mandela kama rais na kiongozi wa
ANC
Kando na kuwa kiongozi anayependwa zaidi duniani, pia aliweza kuonekana
na mitindo ya kipekee kwa sababu ya T sheti zake nzuri nzuri. Hapa
anawaluiza wandishi wa habari maoni yao kuhusu shati yake, baada ya
maankuli ya mchana na muundajji wa mitindo Pierre Cardin
Pia ana mambo mawili ambayo sio kawaida kwa viongozi wa dunia kuwa
nayo....mpole na mwenye kuweza hata kujicheka , hapa anakutana na
mwanamfalme Prince Charles na wanamuziki wa iliyokuwa bendi ya Spice
Girls
Baada ya kutalakiana na mkewe Winnie , Mandela alimuoa Graca Machel,
alipokuwa anasherehekea miaka 80 mwaka 1998. Bi Machel ni mjane wa
aliyekuwa rais wa Msumbiji Samora Machel. Bi Graca na Mandela
walianzisha hazina ya kuwasaidia watoto wasio na uwezo mkubwa maishani
Tangu kuondoka mamlakani, mwaka 1999, bwana Mandela alikuwa mmoja wa
viongozi wakuu kufanya kampeini dhidi ya ukimwi na utovu wa usalama
wakati nchi yake ilipokuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010
Mwaka 2004, akiwa na umri wa miaka 85, Mandela alistaafu kutoka majukumu
ya umma ili kuwa na muda na faimlia yake pamoja na marafiki zake.
Bwana Mandela, aliweza kujitokeza wakati wa sherehe ya kufunga michuano
ya kombe la dunia mwaka huo. Hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya na
alikuwa anaomboleza kifo cha kitukuu wake aliyeuawa huku michuano hiyo
ikianza.
Rais Obama alivyotikisa Msibani Afrika kusini katika kuenzi Mandela
Licha
ya kuwa ni siku ya huzuni kwa dunia nzima, hotuba ya Rais wa Marekani,
Barack Obama imewagusa maelfu ya watu waliokuwa kwenye Uwanja wa FNB
katika ibada ya kitaifa kumwaga Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela.
Obama
aliyetumia dakika 20 katika hotuba yake iliyokuwa ikikatizwa na kelele
za kumshangilia, aliwataka vijana wa Afrika na dunia nzima kuiga maisha
aliyoishi Mandela kama yeye alivyojifunza mambo mengi kutoka kwa
mzalendo huyo.
“Miaka
30 iliyopita nikiwa mwanafunzi, nilisoma Kitabu cha Mandela na tangu
siku hiyo nilijifunza, nikajenga roho ya uthabiti. Iliamsha uwajibikaji
kwa ajili yangu na kwa ajili ya watu wangu… hakika Mandela amenifanya
niwe hivi nilivyo leo. Michelle na mimi tumenufaika sana na Mandela,”
alisema Obama na kuongeza:
“Mandela
alinifanya niwe mtu ninayesimama mbele yenu leo, alichangia kunifanya
kuwa kiongozi bora. Nitaendelea kuiga mfano wake,”
Katika
sherehe hizo, Obama alipokewa kwa shangwe na kushangiliwa kila
alipopita na kila alipozungumza tofauti na ilivyokuwa kwa Rais wa nchi
hiyo, Jacob Zuma ambaye alikuwa akizomewa.
Obama
alimtaja Mandela kama kiongozi anayefaa kuigwa kwani pamoja na kukaa
gerezani kwa miaka 27 akipigania uhuru, hakutaka kung’ang’ania madaraka
na badala yake alistaafu kwa hiari yake, tofauti na viongozi wengi wa
Afrika.
“Mandela
alionyesha uongozi wa vitendo na kujaribu, alikuwa ni mwanamume,
binadamu wa kawaida, mume, baba na kiongozi shupavu,” alisema Obama.
Pia
Obama alisema, Mandela aliachiwa huru kama mfungwa, lakini kama mwalimu
ambaye alitumika kutuonyesha kuwa, ni lazima kuwaamini wenzako ili nao
wakuamini.
“Kufundisha
upatanisho, hakuhitaji kudharau historia mbaya ya nyuma bali ni
kuikabili kwa umakini, ukweli na uhalisia wake. Mandela alibadili
sheria, lakini alibadili mioyo yetu pia,” alisema.
Katika
risala hiyo, Obama alimtaja Mandela kama mwanamapinduzi mkubwa wa karne
ya 20 aliyeibadilisha mioyo ya watu wake, akaimarisha mapatano na
maelewano kwa wazungu na weusi.
“Amezaliwa
kipindi cha Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, kijana aliyekuwa akichunga
ng’ombe na kuteswa na wakubwa zake wa kikabila, lakini ameibuka na kuwa
mwanamapinduzi mkuu wa karne ya 20,” alisema Obama.
Vilevile,
Obama alimfananisha Mandela na Abraham Lincoln, Rais wa zamani wa
Marekani kwa kuiunganisha nchi yake pale ilipokuwa inataka kuvurugika.
Rais
huyo aliufanya umati katika uwanja huo ulipuke zaidi kwa furaha baada ya
kuzungumza neno la Kizulu, ‘ubuntu’ linalomaanisha utu au ubinadamu
ambapo alisema Mandela ameimarisha utu na ubinadamu kwa Waafrika Kusini.
“Alidumisha
‘utu’ miongoni mwetu. Utu ambao tunaweza kuupata kwa kushirikiana na
kuwajali wanaotuzunguka,” alisema Rais huyo ambaye anatajwa kuwa Rais wa
dunia. Obama alionyesha umahiri wake katika risala hiyo na katika
sehemu ya risala hiyo alisema ni wajibu wa kila mmoja kuiga maisha
aliyoishi Mandela.
“Ni lazima tujifunze kutoka kwake, kwa sababu Waafrika Kusini kwa jumla wao wameonyesha kuwa, tunaweza kubadilika.”
Obama
alimtaja Mandela kama mtu asiyependa kujikweza bali aliyeshiriki
kuonyesha mawazo yake na hofu na uhalisia wake hasa kwa kusema kuwa yeye
si mtakatifu labda kama mtakatifu ni sawa na mwenye dhambi ambaye
hachoki kujaribu. Kiongozi huyo alimalizia hotuba hiyo kwa nukuu muhimu
za Mandela zinazosema kuwa, ‘Mimi ni kiongozi wa imani, mustakabali
wangu, na mimi ni nahodha wa roho yangu’ na kuwataka Waafrika Kusini
kuishi katika maneno hayo ya Mandela katika maisha yao.
“Hakika
ilikuwa roho ya ajabu, tutamkumbuka sana. Mungu wabariki Waafrika
Kusini,” alimaliza Obama. Kabla ya hotuba hiyo, Obama alifanya jambo la
kihistoria kwa kupeana mikono na Rais wa Cuba, Raul Castro, kama ishara
ya mapatano baada ya migogoro iliyoko baina ya nchi hizo mbili.
Kabla
ya Obama kuzungumza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika
hotuba yake alisema kuwa, alijitoa muhanga kwa ajili ya usalama, uhuru
na demokrasia ya nchi yake.
“Sherehe
hizi za kumbukumbu zinadhihirisha upinde wa mvua wa taifa. Ninatumaini
tutaweza kuuona upinde huo punde, kupitia mvua ya simanzi,” alisema
Ki-Moon. Ki-Moon alimtaja Mandela kuwa ni kiongozi aliyejiandaa kupoteza
kila kitu kwa ajili ya uhuru na demokrasia.
“Dunia
imepoteza rafiki na mwalimu. Alikuwa ni zaidi ya viongozi wakubwa wa
nyakati zetu; mwalimu mkuu aliyetufundisha kwa mifano,” alisema Ki-Moon.
Wakati
huo huo, Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Thanduxolo Mandela kwa
niaba ya familia ya Mandela alipata nafasi ya kutoa risala yake kwa Rais
huyo na alisema kuwa, familia hiyo ina bahati ya kuwa na mzazi kama
Mandela.
“Utakumbukwa daima, hatuwezi kuusahau mchango wako katika familia na katika maisha ya Waafrika Kusini wote,” alisema Thanduxolo.
Baada
ya Thanduxolo, walikuja wajukuu na vitukuu wa Mandela kwa niaba ya
wajukuu wote, Pumla, Andile na Mbuso Mandela ambao walisema wana mengi
waliyojifunza kwa babu yao ambaye walimtaja kuwa kioo cha familia na
kuahidi kuwa wataishi na matendo yake.
Mandela atazikwa Jumapili.
CHANZO: MWANANCHI
Hali halisi ilivyokuwa jana katika kumbukumbu ya Nelson Mandela
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais
Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa
la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu
ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani,
Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB
jijini Johannesburg.PICHA NA IKULU Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali
mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha
Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na
duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.
Maelfu
kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa
nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee
Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa
rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa
Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013,
alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National
Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na
utawala wa Makaburu.
Baada
ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais
wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela
alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia
kipindi cha pili.
Kiasi
cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo
iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na
majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo
iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.
Mbali
na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine
mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack
Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu
wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu
hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais
watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill
Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani
wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais
Kikwete kesho, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi
wenzake katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa
Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini
ya Union Buildings mjini Pretoria.
Subscribe to:
Posts (Atom)