Na
Theonestina Juma, Kagera
WATAWALA wa
nchi wametakiwa kutosubiri mipango yapangwe hadi yakamilike ya kuvuruga amani
nchini na baadhi ya watu waovu na ndipo waanze kutumia nguvu na gharama kubwa kuyakabili.
Kauli hiyo
imetolewa jana na Paroko Msaidizi wa
Parokia wa Kanisa katoliki Jimbo la
Bukoba ya Bukoba Padri Remigius Rutashubanyuma wakati akihubiri katika misa ya
pili katika kanisa la Bikira Maria wa Huruma mjini Bukoba.
Alisema
matukio yanatokea hapa nchini na yanayozidi kutokea yanapangwa na hivyo watala wala wananchi wasisubiri yatokee
kwani tayari watu wanakuwa wameshapoteza
maisha, huku wengine wakidhurika kwa namna moja ama nyingine .
“Bora kinga
kuliko tiba kamili, tusisubiri tukio litokee ndipo tutumie nguvu na gharama
kubwa kuyakabili, iandaliwe mikakati mizuri ya kuzuia mambo hayo yasitokee, wala yasiendelee
kutokea”.
“Tukisubiri
kukabiliana na majanga ambayo yameshatokea , watu watakuwa wameshapoteza maisha,
wengine watakuwa wamedhurika , huwezi kumpa mtu pole kwa matukio ambayo yanakuwa
yanapangwa heri kulinda usalama wa watu ili kuendelea kudumisha amani”alisisitiza.
Alisema
wakati watawala wanaangalia namna ya kuendelea kulinda usalama wao nao
wanaumini washirikiane nao katika kulinda usalama wa watu wote hasa kwa
kuzingatia ulinzi shirikishi.
Alisema
waumini wa kanisa hilo wasiogope kwenda kanisani kusali kwa kuhofia maisha yao kwani
hata waliouawa na waovu kwa kuwalipuwa na bomu katika kanisa Katoliki parokia
ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti Arusha
waliuawa wakiwa wanamshuhudia kristo.
Alisema
suala matukio yanayoendelea hadi makanisani haijulikani walengwa ni watu gani
hasa, kwani hata kama wanauawa lazima yanamgusa kila mtu hata kama sio wewe
mkristo labda hata ndugu yako na hivyo waumini hao wasiogope kwenda kanisani
kusali.
“Kwa hali
kama hii naamini itafikia hatua waumini wakiogopa kwenda kanisani kusali, mimi
nawaombeni msiogope, kwani huko ndiko kumshuhudia kristo, zingatieni ulinzi
snhirikishi kwani kama ni mipango kama
ya uovu huo lazima unapangwa na ndugu zenu, marafiki zenu, watu wa ukaribu wenu”alisema.
Alisema lazima
watawala waliopewa jukumu la kulinda usalama wa raia wake na mali yao
kuwahakikishia usalama wa watu wake
kwani jukumu waliokabidhiwa ni kulinda amani na utulivu wa nchi na si wakati
matukio ya napangwa wanakaa kimya.
“ Kukaa
kimya ina maana kuwa unakubaliana na hali halisi inayotokea , kwa sababu tukio
kubwa haliwezi kutokea bila kuwepo kwa mipango ya muda mrefu, mipango
yanakuwepo”alisema
Padri huyo
alisema ni jukumu la wanaumini kulinda usalama wao kwani huenda watenda maovu
hao wakawageukia hata waumini na hivyo wanatakiwa kujiamini na kuwa watu wa
ibada muda wote, kwani kizazi cha sasa kinahitaji kufundishwa kwa vitendo zaidi
kuliko maneno .
Aidha aliwataka
waumini wa kanisa hilo kuwa watu wa kujiandaa muda wote , kwani matayarisho ni
muhimu kuliko dhana ya ukristo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment