Monday, May 13, 2013

Bodi ya KCU 1990 LTD yatakiwa kujipanga

Na Theonestina Juma, Kagera
BODI ya  Chama Kikuu  cha Ushirika  ya Kagera Co-operative Union 1990 Ltd (KCU)  imetakiwa kujiboresha ili kuweza kutafuta ni namna gani inavyoweza kwenda kwa wakulima ili kuwapatia  kahawa ya kutosha.
Kauli hiyo imetolewa jana na mmoja wa wajumbe wa Mkutano mkuu wa Mezania wa Chama Kikuu  cha Ushirika wa Kagera 1990 Ltd, Bw. Onesmo Kyaruzi  wa chama cha msingi cha Mutalemwa  katika mkutano wa kujadili mezania ya chama hicho.
Bw. Kyaruzi alisema bodi ya ushirika huo unatakiwa kujiuliza  ni kwa nini  baadhi ya wakulima hawataki kuwapatia kahawa ya kutosha wakati kahawa wanayo.
Alisema “Lazima katika sehemu hii bodi yenyewe ijitathimini kwa nini wanashindwa kwenda kwa wakulima kuzungumza nao ili waweze kuwapatia kahawa ya kutosha, wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini wanashindwa kukusanya kahawa ya kutosha kutoka kwa wakulima, lazima kuna tatizo “.
Alisema si kweli kuwa hakuna kahawa ya kutosha kwa wakulima , bali ipo ya kutosha lakini tatizo lililopo ni kila mwaka wakulima wa zao hilo hawakumbukwi na ushirika kuwaongezea  bei hata  senti moja.
“Jaribuni kuwaongezea   wakulima bei hata senti moja ili iweze kuwa kama kiinua mgongo wao, na si kila mwaka hakuna  hata nyongeza … hawawezi kutoa kahawa yao wako radhi hata kupeleka pengine”alisema .
Hata hivyo kwa upande wa meneja wa Chama  Kikuu cha Ushirika  wa Kagera Co-operative 1990 Bw. Vedasto Ngaiza alisema ongezeko la bei la kahawa inategemeana na hali halisi ya  mnada.
Alisema hali ya biashara ya kahawa itakapoimarika  bei pia itaongezeka tofauti na sasa ambapo alikiri kweli mkulima anayo hali mbaya

No comments:

Post a Comment