NA THEONESTINAJUMA,KAGERA
WAKAZI wa Manispaa ya Bukoba wametakiwa kuwapuuza maneno ya chuki, uchochezi na uchonganishi yanaoenezwa na baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo katika redio za kijamii mjini hapa.
Rai hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema” pamoja na kwamba baadhi ya madiwani hao wamekuwa wakiwahubiria wananchi chuki kupitia kwenye baadhi ya vyombo vya habari mjini hapa, wananchi wanatakiwa kuwapuuza kwani taarifa wanazotoa ni za upuuzi, upotoshaji mkubwa na uliojaa uchonganishi”
Dkt. Amani alisema katika Manispaa hiyo wasemaji wakuu ni yeye na Mkurugenzi wake na si kundi la baadhi ya madiwani waliosaini hati ya kumshtaki ili wamng’oe kwenye nafasi ya umeya ambao wanapinga suala nzima ya maendeleo katika Manispaa hiyo.
Alisema yeye pamoja na wananchi wa Manispaa ya Bukoba na baadhi ya madiwani waliobaki wanaendelea kutekeleza maagizo ya Tume ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda iliotua mjini hapa mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw.Abbas Kandoro ambao waliwataka kuendelea kutumikia wananchi.
“Mimi, wananchi wa Bukoba na baadhi ya madiwani tuliobaki tunaendelea kutekeleza maagizo ya tume ya Waziri Mkuu, na tunaamini kuwa tume bado haijatoa majibu ya uchunguzi wake hivyo tunashangaa wenzetu kwa yote wanayoyafanya”alisema Dkt. Amani
Alisema taangu mwishoni mwa mwezi machi tume ya Waziri Mkuu uondoke mjini hapa hali ilitulia kwa kiasi chake, lakini chokochoko zilianza tena katika kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo iliofanyika Mei 16, mwaka huu.
Alisema katika kikao hicho baadhi ya madiwani saba ambao hawakuhudhuria katika vikao zaidi ya viwili huku baadhi yao wakitoka nje kwenye ajenda ya awali kabisa ya kuthibitisha muhtasari baada ya wengine wakisaini daftari la mahudhurio wakitaka kuthibitisha muhtasari.
“Hivi kweli hili linawezekana, unawezaje kujadili ajenda mbazo zilijadiliwa na wewe haupo… baadhi yao juzi walikuwa wakihoji muhtasari wa kikao kilichopita ambapo kikanuni hawapaswi kushiriki, huwezi kuhoji usahihi wa muhtasari ambao hukushiriki”alisisitiza Dkt. Amani.
“Hata nilipolazimika kuwaambia ukweli huo, walianza kupiga makelele kuwa wanaenda kushtaki kwa Waziri Mkuu Dodoma, nimeambiwa eti wa,eenda madiwani tisa”alisema
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusiana na taarifa zinazodaiwa mjini hapa kuwa tayari yeye anayo majibu ya Tume ya Waziri Mkuu, alisema kuwa si kweli na kwamba majibu hayajatoka bali amekuwa akitekeleza yale walioambiwa na tume kuwa waendelee kuwatumikia wananchi waliowachangua.
“Mimi naendelea kutekeleza yale tulioagizwa na tume, walitutaka tuendelee kuwatumikia wananchi waliotuchagua kwani wanategemea maendeleo kutoka kwetu, na kwamba maendeleo hayo yatawezekana endapo watakuwa wanahudhuria kwenye vikao na matokeo watampatia aliyewatuma”alisema
“Tatizo ni kwamba baadhi ya wawekezaji wananiuliza, hali ikoje kwa sasa katika Manispaa ya Bukoba, nami nawajibu kuwa hali imetulia wanaweza kuanza kuwekeza, kutokana na majibu hayo baadhi ya watu wanatafsiri visivyo”aliongeza.
Dkt. Amani alisema katika vikao vilivyogomewa na madiwani 13 na kusababisha kuahirishwa vilisababishia halmashauri hiyo hasara ya sh. milioni 4,008,500.
Mwisho
No comments:
Post a Comment