Na
Theonestina Juma, Kagera
HALI ya
wakulima wa zao la kahawa katika mkoa wa Kagera unazidi kuwa katika hali mbaya kutokana na taarifa za soko kuonesha kuporomoka katika minada
hasa kwa kahawa aina ya arabika.
Hayo
yamenainishwa jana na Mwenyekiti wa bodi
ya KCU 1990 Ltd, Bw. John Binunshu wakati akitoa taarifa yake katika Mkutano
Mkuu wa 24 wa mwaka uliofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka zaidi ya vyama vya msingi 124 kutoka
katika wilaya za Muleba, Missenyi na Bukoba.
Kutokana na
kupromoka kwa bei ya kahawa katika minada
hasa bei ya kahawa ya Arabica katika iko kati ya dola 1,950 na 2,080
kwa tani au dola 1.95 hadi 2.080.
Kwa mantiki
hiyo Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera
(KCU) 1990 Ltd kimetangaza bei mpya ya
kununulia kahawa kutoka kwa wakulima katika
msimu wa mwaka 2013/2014.
Alisema kwa msimu wa mwaka 2013/2014 bei mpya ya kahawa itakuwa kati ya
sh. 1,000 na 900 kwa kilo.
Akifafanua
zaidi alisema Robusta maganda itanunuliwa kwa sh. 900, Arabika maganda sh.1,000, Arabica
safi 2,100, Robusta safi 1,900 kwa kilo huku Arabica Organic sh. 3,000 ,Robusta
Organic sh. 2,800 na Robusta Organic UG
sh.1,500 kwa kila kilo.
Bw. Binunshu
alisema kwa makisio KCU 1990 Ltd kinatarajia kukusanya tani 7,500 za kahawa
aina zote ambapo kati ya makusanyo hayo tani 2,350 zitakuwa ni za Organic.
Alisema tani
5,150 zitakuwa za kahawa ya kawaida na kwamba kati ya hizo tani 4,554.5
zitakuwa za robusta na tani 595.5 zitakuwa za Arabica.
Katika msimu
wa mwaka 2012/2013 bei ya kahawa aina ya robusta ilikuwa sh.1,350 kwa kilo ambapo bei hiyo ilishuka hadi kufikia sh.1,100
kwa kilo ambapo tena bei hiyo ilipanda na kurudia ile ya awali kutokana na bei
kupanda katika soko la dunia.
Kutokana na
kutokuwepo kwa bei nzuri ya kumridhisha mkulima ibeinisha kuwa ni miongoni mwa
visababishi wa wakulima kuamua kuuza zao hilo kimagendo kwa walanguzi kutoka
nchi jirani ya Uganda, ambao kwa mwaka jana walilangua zao kilo kwa sh. 1,500
kwa kilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment