Sunday, May 26, 2013

Wakati kuolewa na mfalme ni dili Swizeland binti atorokea Uingereza kukwepa ndoa za wake wengi




Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.

Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.

Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.

Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.

Aliongeza: "Alianza kunipigia simu kwenye shule ya bweni. Aliniuliza kama ningetaka kuwa sehemu ya familia ya kifalme. Ilinibidi kukaa kimya kuhusu mashaka yangu lakini nilifahamu sikutaka kuolewa naye na kujitolea maisha yangu kwa mfalme huyo.


"Wake zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."

Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.

"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."

Tangu kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au kushambuliwa.

Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."

Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007 kukataliwa mwaka 2011.

Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.

Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.

Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."

Baba huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya joto mwaka jana.

Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili' uliofanywa na mume wake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.

Meya Bukoba awashangaa madiwani 9 kukimbilia kwa Waziri Mkuu kumshtaki

NA THEONESTINAJUMA,KAGERA
WAKAZI wa Manispaa ya Bukoba wametakiwa kuwapuuza maneno ya chuki, uchochezi  na uchonganishi yanaoenezwa na  baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo katika redio za kijamii mjini hapa.
Rai hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema” pamoja na kwamba baadhi ya madiwani hao wamekuwa wakiwahubiria wananchi chuki kupitia kwenye baadhi ya vyombo vya habari mjini hapa, wananchi wanatakiwa kuwapuuza kwani taarifa wanazotoa ni za upuuzi, upotoshaji mkubwa na uliojaa uchonganishi”
Dkt. Amani alisema katika Manispaa hiyo wasemaji wakuu ni yeye na Mkurugenzi wake na si kundi la  baadhi ya madiwani waliosaini hati ya kumshtaki ili wamng’oe kwenye nafasi ya umeya ambao wanapinga suala nzima ya maendeleo katika Manispaa hiyo.
Alisema yeye pamoja na wananchi wa Manispaa ya Bukoba na baadhi ya madiwani waliobaki wanaendelea kutekeleza maagizo ya Tume ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda iliotua mjini hapa mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw.Abbas Kandoro ambao waliwataka kuendelea kutumikia wananchi.
“Mimi, wananchi wa Bukoba na baadhi ya madiwani tuliobaki tunaendelea kutekeleza maagizo ya tume ya Waziri Mkuu, na tunaamini kuwa tume bado haijatoa majibu ya uchunguzi wake hivyo tunashangaa wenzetu kwa yote wanayoyafanya”alisema Dkt. Amani
Alisema taangu mwishoni mwa mwezi machi tume ya Waziri Mkuu uondoke mjini hapa hali ilitulia kwa kiasi chake, lakini  chokochoko zilianza tena katika kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo iliofanyika Mei 16, mwaka huu.
Alisema katika kikao hicho baadhi ya madiwani saba ambao hawakuhudhuria katika vikao zaidi ya viwili huku baadhi yao wakitoka nje kwenye ajenda ya awali kabisa ya kuthibitisha muhtasari baada ya wengine wakisaini daftari la mahudhurio wakitaka kuthibitisha muhtasari.
“Hivi kweli hili linawezekana, unawezaje kujadili ajenda mbazo zilijadiliwa na wewe haupo… baadhi yao juzi walikuwa wakihoji muhtasari wa kikao kilichopita ambapo kikanuni hawapaswi kushiriki, huwezi kuhoji usahihi wa muhtasari ambao hukushiriki”alisisitiza Dkt. Amani.
“Hata nilipolazimika kuwaambia ukweli huo, walianza kupiga makelele kuwa wanaenda kushtaki kwa Waziri Mkuu Dodoma, nimeambiwa eti wa,eenda madiwani tisa”alisema
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusiana na taarifa zinazodaiwa mjini hapa kuwa tayari yeye anayo majibu ya Tume ya Waziri Mkuu, alisema kuwa si kweli na kwamba majibu hayajatoka bali amekuwa akitekeleza yale walioambiwa na tume kuwa waendelee kuwatumikia wananchi waliowachangua.
“Mimi naendelea kutekeleza yale tulioagizwa na tume, walitutaka tuendelee kuwatumikia wananchi  waliotuchagua kwani wanategemea maendeleo kutoka kwetu, na kwamba maendeleo hayo yatawezekana endapo watakuwa wanahudhuria kwenye vikao  na matokeo watampatia aliyewatuma”alisema
“Tatizo ni kwamba baadhi ya wawekezaji wananiuliza, hali ikoje kwa sasa katika Manispaa ya Bukoba, nami nawajibu kuwa hali imetulia wanaweza kuanza kuwekeza, kutokana na majibu hayo  baadhi ya watu wanatafsiri visivyo”aliongeza.
Dkt. Amani alisema katika vikao vilivyogomewa na  madiwani 13 na kusababisha kuahirishwa  vilisababishia halmashauri hiyo hasara ya sh. milioni 4,008,500.
Mwisho

Wednesday, May 15, 2013

Huzuni kwa wauza magazeti Kagera , waondokewa na kipenzi chao, Bw. Benezeth



Na Theonestina Juma, Kagera
WAUZAJI wa magazeti katika Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera wamepata pigo kubwa baada ya mwenzao  Bw. Benezeth Kamigan Barnabas (47) kufariki dunia baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa kuoza sehemu ya utumbo mpana.
Kijana wa marehemu, Bw. Benson Kamigan aliyekuwa akimuuguza baba yake katika hospitali ya Mkoa Kagera katika wodi namba moja alikokuwa amelazwa, alisema baba yake alikata roho  jumanne wiki hii, Mei 14, mwaka huu saa 11 jioni mara baada ya kufanyishwa mazoezi ya kutembea.
Alisema baba yake alikimbizwa katika hospitali ya Mkoa Kagera, Mei 2 mwaka huu  usiku wa manane baada ya kulalamikia kusokotwa na tumbo la ghafla.
Alisema kutokana na hali hiyo, Mei 3, mwaka huu baba yake alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa kipande cha utumbo wake mpana umeoza.
Hivyo siku hiyo alifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuondolewa kipande wa utumbo huo uliokuwa na urefu wa nusu mita.
Hata hivyo, tangu baba yake afanyiwe upasuaji huo, upumuaji wake ulikuwa wa kuhema hema, kwani ilionekana wazi kuwa pumzi ulikuwa si wa kutoka ndani ya tumbo zaidi ya kifuani pekee.
Jumanne wiki hii hali ya baba yake ilibadilika ghafla mara baada ya kutoka kumfanyisha mazoezi ya kutembea kulingana na maelezo aliokuwa akipewa na madaktari kwa ajili ya kujiandaa kuondolewa nyuzi ambapo jioni saa 11 mara tu baada ya mazoezi alikata roho.
“Jioni hii nilikuwa namfanyisha baba mazoezi ya kutembea, lakini tuliporea ndani ya wodi alilala kitandani mara akaanza kutokwa mapovu mdomoni na kutapatapa  kama dakika 15 hivi na kisha akakata roho”alisema Bw. Benson.
Bw. Benezeth aliwahi kuwa wakala wa magazeti ya kampuni ya Business Times Ltd kati ya mwaka 1996  mkoani Kagera na baadaye mwaka 2003 alianza kujikita rasmi katika uuzaji wa magazeti.
Marehemu anatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda kuzikwa kijijini kwake Bulembo kata ya Kamachumu Wilayani Muleba.
Bw. Benezeth ameacha mjane watoto saba wakike wakiwa wanne na kiwemo mtoto mchanga wa miezi mitatu na wakiume wakiwa ni watatu.
Mwisho.

Bei ya kahawa yazidi kuliza wakulima Kagera



Na Theonestina Juma, Kagera
HALI ya wakulima wa zao la kahawa katika mkoa wa Kagera unazidi kuwa katika hali  mbaya kutokana na taarifa  za soko kuonesha  kuporomoka  katika minada  hasa kwa kahawa aina ya arabika.
Hayo yamenainishwa jana na Mwenyekiti wa  bodi ya KCU 1990 Ltd, Bw. John Binunshu wakati akitoa taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa 24 wa mwaka uliofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na wajumbe  kutoka zaidi ya vyama vya msingi 124 kutoka katika wilaya za Muleba, Missenyi na  Bukoba.
Kutokana na kupromoka kwa bei ya kahawa katika minada  hasa  bei ya kahawa  ya Arabica katika iko kati ya dola 1,950 na 2,080 kwa tani au dola 1.95  hadi 2.080.
Kwa mantiki hiyo  Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera  (KCU) 1990 Ltd kimetangaza bei mpya ya kununulia kahawa kutoka kwa wakulima  katika msimu wa mwaka 2013/2014.
Alisema  kwa msimu wa mwaka  2013/2014 bei mpya ya kahawa itakuwa kati ya sh. 1,000  na 900 kwa kilo.
Akifafanua zaidi alisema Robusta maganda itanunuliwa kwa  sh. 900, Arabika maganda sh.1,000, Arabica safi 2,100, Robusta safi 1,900 kwa kilo huku Arabica Organic sh. 3,000 ,Robusta Organic  sh. 2,800 na Robusta Organic UG sh.1,500 kwa kila kilo.
Bw. Binunshu alisema kwa makisio KCU 1990 Ltd kinatarajia kukusanya tani 7,500 za kahawa aina zote ambapo kati ya makusanyo hayo tani 2,350 zitakuwa ni za Organic.
Alisema tani 5,150 zitakuwa za kahawa ya kawaida na kwamba kati ya hizo tani 4,554.5 zitakuwa za robusta na tani 595.5 zitakuwa za Arabica.
Katika msimu wa mwaka 2012/2013 bei ya kahawa aina ya robusta ilikuwa sh.1,350 kwa kilo  ambapo bei hiyo ilishuka hadi kufikia sh.1,100 kwa kilo ambapo tena bei hiyo ilipanda na kurudia ile ya awali kutokana na bei kupanda katika soko la dunia.
Kutokana na kutokuwepo kwa bei nzuri ya kumridhisha mkulima ibeinisha kuwa ni miongoni mwa visababishi wa wakulima kuamua kuuza zao hilo kimagendo kwa walanguzi kutoka nchi jirani ya Uganda, ambao kwa mwaka jana walilangua zao kilo kwa sh. 1,500 kwa kilo.
Mwisho.

Monday, May 13, 2013

Bodi ya KCU 1990 LTD yatakiwa kujipanga

Na Theonestina Juma, Kagera
BODI ya  Chama Kikuu  cha Ushirika  ya Kagera Co-operative Union 1990 Ltd (KCU)  imetakiwa kujiboresha ili kuweza kutafuta ni namna gani inavyoweza kwenda kwa wakulima ili kuwapatia  kahawa ya kutosha.
Kauli hiyo imetolewa jana na mmoja wa wajumbe wa Mkutano mkuu wa Mezania wa Chama Kikuu  cha Ushirika wa Kagera 1990 Ltd, Bw. Onesmo Kyaruzi  wa chama cha msingi cha Mutalemwa  katika mkutano wa kujadili mezania ya chama hicho.
Bw. Kyaruzi alisema bodi ya ushirika huo unatakiwa kujiuliza  ni kwa nini  baadhi ya wakulima hawataki kuwapatia kahawa ya kutosha wakati kahawa wanayo.
Alisema “Lazima katika sehemu hii bodi yenyewe ijitathimini kwa nini wanashindwa kwenda kwa wakulima kuzungumza nao ili waweze kuwapatia kahawa ya kutosha, wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini wanashindwa kukusanya kahawa ya kutosha kutoka kwa wakulima, lazima kuna tatizo “.
Alisema si kweli kuwa hakuna kahawa ya kutosha kwa wakulima , bali ipo ya kutosha lakini tatizo lililopo ni kila mwaka wakulima wa zao hilo hawakumbukwi na ushirika kuwaongezea  bei hata  senti moja.
“Jaribuni kuwaongezea   wakulima bei hata senti moja ili iweze kuwa kama kiinua mgongo wao, na si kila mwaka hakuna  hata nyongeza … hawawezi kutoa kahawa yao wako radhi hata kupeleka pengine”alisema .
Hata hivyo kwa upande wa meneja wa Chama  Kikuu cha Ushirika  wa Kagera Co-operative 1990 Bw. Vedasto Ngaiza alisema ongezeko la bei la kahawa inategemeana na hali halisi ya  mnada.
Alisema hali ya biashara ya kahawa itakapoimarika  bei pia itaongezeka tofauti na sasa ambapo alikiri kweli mkulima anayo hali mbaya

Msisubiri majanga yatokee ndipo mtumie nguvu na gharama kubwa kuyakabili-Padri,ataka waumini wasiopoge kwenda kusali makanisani, waliofariki kwa bomu walikuwa wakishuhudia kristo



Na Theonestina Juma, Kagera
WATAWALA wa nchi wametakiwa kutosubiri mipango yapangwe hadi yakamilike ya kuvuruga amani nchini na baadhi ya watu waovu na ndipo waanze kutumia  nguvu na gharama  kubwa kuyakabili.
Kauli hiyo imetolewa  jana na Paroko Msaidizi wa Parokia  wa Kanisa katoliki Jimbo la Bukoba ya Bukoba Padri Remigius Rutashubanyuma wakati akihubiri katika misa ya pili katika kanisa la Bikira Maria wa Huruma mjini Bukoba.
Alisema matukio yanatokea hapa nchini na yanayozidi kutokea yanapangwa  na hivyo watala wala wananchi wasisubiri yatokee kwani  tayari watu wanakuwa wameshapoteza maisha, huku wengine wakidhurika kwa namna moja ama nyingine .
“Bora kinga kuliko tiba kamili, tusisubiri tukio litokee ndipo tutumie nguvu na gharama kubwa kuyakabili, iandaliwe mikakati mizuri ya kuzuia  mambo hayo yasitokee, wala yasiendelee kutokea”.
“Tukisubiri kukabiliana na majanga ambayo yameshatokea , watu watakuwa wameshapoteza maisha, wengine watakuwa wamedhurika , huwezi kumpa mtu pole kwa matukio ambayo yanakuwa yanapangwa heri kulinda usalama wa watu ili kuendelea kudumisha amani”alisisitiza.
Alisema wakati watawala wanaangalia namna ya kuendelea kulinda usalama wao nao wanaumini washirikiane nao katika kulinda usalama wa watu wote hasa kwa kuzingatia ulinzi shirikishi.
Alisema waumini wa kanisa hilo wasiogope kwenda kanisani kusali kwa kuhofia maisha yao kwani hata waliouawa na waovu kwa kuwalipuwa na bomu katika kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi  Olasiti Arusha waliuawa wakiwa wanamshuhudia kristo.
Alisema suala matukio yanayoendelea hadi makanisani haijulikani walengwa ni watu gani hasa, kwani hata kama wanauawa lazima yanamgusa kila mtu hata kama sio wewe mkristo  labda hata ndugu yako  na hivyo waumini hao wasiogope kwenda kanisani  kusali.
“Kwa hali kama hii naamini itafikia hatua waumini wakiogopa kwenda kanisani kusali, mimi nawaombeni msiogope, kwani huko ndiko kumshuhudia kristo, zingatieni ulinzi snhirikishi kwani kama ni  mipango kama ya uovu huo lazima unapangwa na ndugu zenu, marafiki zenu, watu wa ukaribu wenu”alisema.  
Alisema lazima watawala waliopewa jukumu la kulinda usalama wa raia wake na mali yao kuwahakikishia usalama  wa watu wake kwani jukumu waliokabidhiwa ni kulinda amani na utulivu wa nchi na si wakati matukio  ya napangwa wanakaa kimya.
“ Kukaa kimya ina maana kuwa unakubaliana na hali halisi inayotokea , kwa sababu tukio kubwa haliwezi kutokea bila kuwepo kwa mipango ya muda mrefu, mipango yanakuwepo”alisema
Padri huyo alisema ni  jukumu la wanaumini  kulinda usalama wao kwani huenda watenda maovu hao wakawageukia hata waumini na hivyo wanatakiwa kujiamini na kuwa watu wa ibada muda wote, kwani kizazi cha sasa kinahitaji kufundishwa kwa vitendo zaidi kuliko maneno .
Aidha aliwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watu wa kujiandaa muda wote , kwani matayarisho ni muhimu kuliko dhana ya ukristo.
Mwisho.

Friday, May 10, 2013

Serikali kupambana na kundi ndogo la wachochezi wa kidini nchini-Pinda

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/05/IMG_0607.jpg
WAZIRI mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya kushughulika na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa kidini ambao unachangia kudhoofisha amani ya nchi.
“Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, msishangae kuona watu wanawahoji lakini kwa nia njema, ya kurudisha amani yetu,” Alisema mheshimiwa Pinda.
Mh. Pinda Ametoa kauli hiyo leo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi,
Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na
mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.
Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.
“Ninawaomba Watanzania tushirikiane kuwafichua watu hawa waovu kwa sababu tunaishi nao, ni watu ambao wako miongoni mwetu… Tusaidieni kutunong’oneza ili tuchukue hatua”, . Alisisitiza mh. Pinda.
Waziri Mkuu alisema yeye ni miongoni mwa watu wanaoamini kwamba ukristo au uislamu hauwezi kuondolewa kwa kuwaua viongozi wa dini au waumini wao. “Ni kujidanganya tu mtu akiamini kuwa akimuua Askofu,Mufti au  Muumini ataimaliza dini yoyote. Madhehebu haya mawili ni nguzo kubwa kwa Taifa letu, tunatamani tuendelee kuwa na amani iliyokuwepo siku zote,” alisisistiza Mh. Pinda.
 Alisema Serikali kupitia idara ya maafa itatoa sh. milioni 100/- ili zisaidie kukabiliana na janga lililowakabili wana Arusha.
Mapema, akiongoza ibada hiyo, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo aliwataka waumini wote kutolipa uovu kwa uovu bali watende wema ili kusahihisha maovu. “Ishara ya uovu imetendwa na hawa watu dhidi ya waumini wenzetu kwa madhumuni yanayojulikana na wao tu bila kuchokozwa
na hawa marehemu ama wale waliko hospitali (majeruhi),” alisema.
“Uovu umeshatendwa, je sisi tufanye nini? Angekuja hapa kanisani Yule aliyesababisha mauti haya, tungemfanya nini?” Alihoji Kardinali Pengo na kujibiwa na mamia ya waumini waliohudhuria ibada hiyo: “Tungemsamehe.”
Aliwasihi waumini wote kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania ili tukio hilo na lile la kuuawa kwa Padre Evarist Mushi kule Zanzibar yasiwe sababu ya kusambaratika kwa amani ya Taifa hili.
“Tusilipe ubaya kwa ubaya, tuendelee kuomba Mungu asikie sala yetu na awazindue wenye mamlaka watimize wajibu wao,” alisema.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), alilaani waliosababisha mauaji hayo na kusema kitendo hicho kimelitia doa Taifa kwa vile ni kitendo kinachoashiria kuchafua amani ya Tanzania.
Aliwasihi waumini wote kutokuwa waoga katika kazi ya kumtangaza Kristo. “Risasi zinapigwa, mioto inayowashwa katika makanisa yetu na mabomu yanayolipuliwa yasiwe sababu ya kututia hofu. Imani yetu haiku katika miili bali iko mioyoni mwetu,” alisema.
Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha akitoa shukrani kwa
niaba ya Kanisa Katoliki aliwashukuru wote waliofika kuwafariji
kutokana na tukio hilo na kuwathibitishia kuwa kama Kanisa wameguswa
na moyo waliouonyesha.
Watu 66 waliathirika kutokana na mlipuko huo uliotokea Mei 5, mwaka huu ambapo watatu wamefariki dunia na kati ya wagonjwa 63 waliobakia, wanane walihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, wengine waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, na baadhi wanaendelea kupatiwa matibabu
mjini Arusha.

Hali halisi ilivyokuwa katika mazishi ya waliouawa kwa bomu Arusha hivi leo, ni huzuni tupu

Majeneza yakiwa kanisani kabla ya ibada ya mazishi
Mapadri wakiwa wamebeba moja ya majeneza
Baadhi ya Watawa wakiwa kanisani wakati wa ibada
Viongozi wa Kanisa wakitoa salamu za mwisho
Kilio anamlilia mama yake mzazi

Wananchi wakitoa salamu zao za mwisho.
Majonzi, kweli inauma.
Wahudumu wakishusha mwili wa marehemu kaburini kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Wahudumu wakishusha mwili wa marehemu kaburini kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha

Baadhi ya maaskofu kutoka majimbo mbalimbali waliohudhuria ibada ya mazishi leo
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT),Dk Alex Malasusa(kushoto)akiwa na viongozi wengine wa Kanis a hilo wakiwa kwenye ibada ya mazishi
Sehemu ya moja ya umati wa watu waliohudhuria maziko hayo
Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa(kulia)akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk Emmanuel Nchimbi kabla ya ibada kuanza

Rais Kikwete awafariji wafiwa wa mlipuko wa bomu Arusha

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,

Wednesday, May 8, 2013

Magaidi walipua kanisa Katoliki Arusha




DSCN2227Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
DSCN2220Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
DSCN2228Ulinzi umeimarishwa
DSCN2252Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DSCN2246Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
DSCN2282Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
DSCN2258Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
DSCN2273Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
DSCN2236Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
DSCN2251
DSCN2267Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
DSCN2276
DSCN2255
DSCN2281
DSCN2225
DSCN2222
DSCN2215
DSCN2218
DSCN2219
You might also like: