Hapa mbele ya kanisa la TAG Hamugembe kila mtu akiwa anatafakari lake
Katikati ni Mchungaji Vicent Chacha akiwa katika tafakari na baadhi ya wachungaji wenzake baada ya kutoa heshima zao za mwisho
Watu wakiwa wamepanga mstari kwa lengo la kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao Askofu Kabuga
Wengine wakiwa ndani wanakaribia kuaga mwili huo
Wanakwaya wa TAG Hamugembe wakiwa wanaimba kwa huzuni wakati wa kuagwa kwa mwili wa Askofu wao Kabuga
Kijana wa Askofu Kabuga, Bw. Christopher akitoa heshima zake za mwisho |
Msafara wa magari yakitoka kanisani hapo yakielekea kwake marehemu Kagondo |
Jeneza lililobeba mwili wa Askofu Kabuga likiwa linaondolewa kanisani TAG Hamugembe kwa lengo la kupelekwa kwake Kagondo kwenye nyumba yake ya milele.
Hapa kila mtu alikuwa na kazi yake maalum, angalia mwenyewemama mzazi wa Askofu huyo aliyeshika tama akiwa pamoja na mjane wa Askofu Kabuga tayari kuelekea Kagondo kupumzisha mwili wa mpendwa wao
Binti wa Askofu Kabuga ambaye jina lake halikupatikana mara moja alianguka ndani ya kanisa wakati akitoa heshima za mwisho mwili wa baba yake, akiwa anasaidiwa.
Mama wa Askofu Kabuga akitoka kutoa haeshima za mwisho kwa mwanaye
Baadhi ya waumini wa TAG wakiwa wamejawa na huzuni mara baada ya kutoa heshima zao za mwisho
Ndugu yangu usafiri nao ulikuwa tete kila mmoja alitaka kuopanda hili lori lililokuwa limebeba wapuliza tarumbeta
No comments:
Post a Comment