Mtuhumiwa
wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani Tarime mkoani Mara,
aliyekuwa akihojiwa Polisi kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili,
amefariki katika Hospitali ya Wilaya wakati akipatiwa matibabu ya
ugonjwa wa pumu.
Kamanda
wa Polisi Tarime na Rorya, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, alisema
kuwa mtuhumiwa huyo jina lake halisi ni Charles Kichune (38) na
alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akitibiwa ugonjwa huo
hospitalini.
Majina mengine aliyokuwa akiyatumia kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha ni pamoja na Josephat Chacha na Charles Msongo.
"Mwili wa
marehemu upo chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ukisubiri
kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake," alisema Kamanda
Kamugisha.ANGALIA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment