Na Theonestin Juma
CHAMA cha
mapinduzi taifa kimesema mgogoro wa kisiasa katika Manispaa ya Bukoba umevuka mpaka wa Chama na
hivyo kimemwangiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia wizara ya Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kuunda tume kutoka wizarani ili kuja Bukoba kuchunguza tuhuma zinazoelekezwa
kwa Meya wa Manispaa hiyo, Dkt. Anatory Amani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) itikati na uenezi taifa, Nape Nnauye wakati akizungumza na
waandishi wa habari uwanja wa ndege
mjini hapa akiwa safarini kuelekea Jijini Dar Es Salaam baada ya kufanya ziara
yake siku moja mjini hapa baada kusikia
mgogoro unaondelea ndani ya manispaa hiyo ya baadhi ya madiwani kususia vikao
na hivyo kuathiri utendaji ndani ya manispaa hiyo.
Nnauye alisema mgogoro ulipo katika manispaa
ya Bukoba umevuka mpaka na hivyo inahitajika serikali kuu kuingilia kati.
Alisema mgogoro
huo umeathiri vikao vingi vya CCM, jambo ambalo amesema kuwa limesikitisha
chama hicho taifa na hivyo kuhitajika nguvu za ziada kuondoa mgogoro huo.
Alisema
katika mazungumzo yao na baadhi ya madiwani hao wametakiwa kurudi na kufanya
vikao kama kawaida kwa maendeleo ya
jamii kulingana na utaratibu na kanuni za Manispaa hiyo.
Alisema CCM
taifa kinasikitishwa na kufedheheshwa na mgogoro unaoendelea katika manispaa ya
Bukoba, kwani hauna tija kwa yeyote, wala kwa chama, kwa wananchi hata kwa watu
wanaoshikiriki katika mgogoro huo.
Alisema kuna
tuhuma nyingi ya Meya kuhusiana na soko, kituo cha mabasi, viwanja na
uendeshaji wa halmashauri na hivyo tume ikija inayo mamlaka ya kuchunguza na
kutoa taarifa.
Alisema
taarifa ya tume hiyo ikiamilika itawekwa hadharani kwa sababu maneno hayo
yametoka ndani na kwa sasa yako nje kwa hiyo ni vizuri wananchi wakajua.
Alisema
wakati wa kuchunguza wanayo mamalka kama tume pamoja na mambo mengine wanaweza
kulazimika kusimamisha baadhi ya watu kwa ajili ya kupisha uchuguzi huo lakini
wao wataangalia sheria zinasemaje.
Kuhusiana na
vipeperushi vinavyoendelea kutolewa mjini hapa alisema kuwa vipeperushi hivyo
vimekuwa vikigawa wananchi na viko katika mrengo wa kugawa watu kidini.
Alisema
kutokana na vipeperushi hivyo, chama hicho kimeagiza serikali kuwatafuta watu
wanaotengezeza vipeperushi hivyo ili kuweza kuchukuliwa hatua na kuwa anamaamii
kuwa hakuna atakayepona katika hilo hata kama ni wanachama wa CCM
“Hatuwezi kuvumilia
masuala kama haya, kama ni wanachama wetu lazima tutawachukuliwa hatua za kinidhamu
kulingana na chama cha CCM”alisema
Kuhusu
baadhi ya madiwani kuwekwa mfukoni na baadhi ya watu, alisema mgogororo huo
umevuka mpaka wa chama ndiyo sababu wamweo mba tume inge ichunguze suala hilo.
“Mgogoro huu
ulikofikia kwa sasa umevuka mpaka wa chama ndiyo sababu sasa tunataka tume ije
ichungue mambo kama hayo ya baadhi ya mafiwani kuwekwa ndani ya mfuki wa mtu,
wao ndiyo watatuambia ukweli, ama hawa madiwani wanaamua kufanya hivhyo kwa
utashi wao’alisema Nnauye.
Tume
utagundua kama kuna fedha zimechakachuliwa, au msingi wa mgogoro huu ni nini,
hiyo timu inatao majibu yake.
Kuhusu athari
ambayo mgogoro huo umeleta ndani ya chama Bw. Nnauye alisema kuwa ni pamoja na
chama sio kitu kimoja , watu wamegawanyika, nah ii ni kutojna na madiwani wa
CCM ndiyo wengi,
Halikadhalika
alisema mgogoro huo umeathiri utekelezaji wa ilani ya ccm ya uchaguzi mwaka 2010
kwa sababu bajeti isipotishwa pesa hazitatoka kwa wakati na hivyo miradi mingi
itakwama, kuanza kutekelezwa, pia waathirika wakubwa ni wananchi, mfano kama
huduma ya maji , madawa, shule zitakosekana.
‘Kutokana na
hali hii, ndiyo maana kwa sasa inahitajika nguvu kubwa, … zaidi itumike ili
kumaliza mgogoro huu, kwani utaathiri utekelezaji wa ilani ya uchanguzi wa CCM “alisema
Alisema
mgogoro huo ndiyo chanzo cha kuzaa vipeperushi vilivyozaa mitaani ya unalenga kugawa wananchi wa manispaa ya
Bukoba. Na ndiyo maana vikao vikitaka kufanyika watu hudhuria ili kuja
kuangalia kwa sababu watu wamegawanyika.
“Tumeigawa
jamii yetu kutokana na mgogoro huu, unakuta kundi moja linapita upende mwingine
na lingine upande moja wanaanza kuzomeana, tukiendelea hivyo wanaishi kama watu ambao si wa eneo moja, si watu ambao
walikuwa wanakubalina, litafanya Bukoba lisiwe eneo nzuri la kuja kupumzika”alisema
Alisema wakati
mgogoro huo unaanza si kweli kuwa Chama kilikaa kimya bali kuna hatua
zilizochukuliwa na kwamba si kwamba kila mgogoro unapoanza lazima CCM taifa liingilie
kati, bali pale ambapo ngazi ya chini inaposhindwa ndipo taifa huingilia kati.
“Sisi hatuna
utamaduni wa kuhamisha babu na vijukuu katika sehemu moja ya migogoro kama
ilivyo kwa wapinzani wetu, sisi tunautaratibu wetu,… sisi sio chama cha
harakati … sisi tunautaratibu wa kushughulikia migogoro”alisema
Mgogoro
ndani ya chama ikizimgatiwa kuwa mwaka 2014 wanaingia katika uchanguzi wa
serikali za mitaa, alisema kuwa sehemu ambapo kuna mgogoro ni afya .
Alisema malumbano
na mvutano huo unatewgemea pia kutofautiana kule unahitimishwaje , hivyo kuamua
watashindishaje ni kuangalia ni ni namna walvyotafautiana.
Alisema “wenzetu
wale ambao ni wapinzani wetu wasubiri tu ushindi wa kibunga 2015, kwani watu
wamewachoka na wamewaona walivyo wakiwa bungeni.
Aidha aliwapa
ushauri wapinzani kuwa miaka mingi Tanzania
wamekuwa na vyama vya upinznai vya kukosa na sio kuelekeza na kuleta sera
mbadala.
Katika mfumo
wa vyama vingi ukiwa na vyama vya nam,na hiyo, vitabaki kuwa vya upinzani kwa muda mrefu kwa sababu wao
wakikosoa wao wanakwenda kurekebisha na wananchi wanazidi wakuwapenda.
Ukitaka
kushika dola toa kitu mbadala wenzao wanafanya A’ wewe sema ukipewa madaraka
utafanya B’ haitoshi kukosoa A peke yake bila kutoa mbadala sasa wenzetu kwa
utaratibu huu tunawaombea maisha mema ya kuendelea kuwa wapizani, wafanye kazi
nzuri ya kutukosoa ,ya kupiga kelele, kupata ruzuku kwa sababu ndiyo wanayoitaka
na sisis tumepewa kazi ya kupanga mikakati ya maendeleo”alisema
Mwisho.
No comments:
Post a Comment