Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akienda kusoma Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kat
No comments:
Post a Comment