Saturday, June 29, 2013

Maajabu ya tango katika afya ya mwanandamu



 
Hawakukosea wale waliosema  kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako.  Matunda mengi yana manufaa lakini tango tunasema limetia fora.
 Kwanza linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc.
Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.
 Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.
Nne, unataka kuondoa ‘hangover’ au maumivu makali ya kichwa, kula tango ambalo lina sukari ya kutosha na vitamin zitakazoweka mambo sawa mwilini.
 Tano, umechelewa kwenda kwenye usaili, viatu ni vichafu, chukua vipande vya tango na sugulia katika viatu. Vitang’aa.
Sita, umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya  mdomo.
Saba, midomo imekauka na inauma? Chukua kipande cha tango na sugulia mdomoni,  utaona mabadiliko katika midomo.
 Nane, umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane.
 Tisa, umekosea kuandika katika ubao au ukuta, chukua maganda ya tango na usugulie taratibu, wino au rangi hiyo itafutika kabisa.
 Kumi, pia, tango lina uwezo mzuri wa kusafisha vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu au maji ya chumvi.
0
Share




No comments:

Post a Comment