Wednesday, November 26, 2014

Ripoti ya ESCROW yatikisa nchi, inasikitisha!!

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akienda kusoma Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kat

Friday, November 21, 2014

Mapinduzi KCU 1990, Wajumbe wa bodi wa zamani wote watupwa wachaguliwa sura mpya






Pichani ni wajumbe saba waliochaguliwa leo katika Uchaguzi Mkuu maalum uliofanyika mjini  Bukoba, ambapo mwenyekiti mpya ni Bw. Frank Muganyizi mwenye masters ya Uchumi.

Wednesday, November 19, 2014

Majonzi Bukoba, Mfanyabiashara Maarufu afia ndani ya gari akifanya mapenzina msichana



Na Theonestina Juma,Bukoba
 MFANYABIASHARA  maarufu  mjini  Bukoba Mkoani Kagera, Bw.Leonard Mtensa (50) amefariki  dunia ghafla  wakati  akifanya mapenzi na mwanamke mmoja  ndani ya  gari  lake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mjini hapa na kusambaa kila kona ya mji wa  Bukoba nakuthibitishwa na  Kamanda wa polisi Mkoa Kagera Henry Mwaibambe ,tukio hilo la aina yake limetokea Novemba 18,mwaka huu saa 4.00 usiku katika maeneo ya Buyekera mjini Bukoba
Kamanda  Mwaibambe,alisema mfanyabiashara huyo ni  mmiliki wa klabu  maarufu  ya   usiku  Bukoba   iitwayo  Linas night club.
Alisema kabla ya   kufikwa  na  umauti  mfanyabiashara huyo  alikuwa akifanya mapenzi ndani ya gari  lake  lenye namba za usajili T.982 CQG  aina  ya IST.
Alimtaja msichana aliyekuwa akifanya mapenzi na mfanyabiashara huyo kuwa ni Bi. Jackline  Hassan (25 )  mkazi wa Buyekera.
Alisema  wakati  wapenzi  hao  wakiendelea  na mapenzi  ghafla   hali   ya mfanyabiashara  huyo   ilibadilika  na kukimbizwa   katika  kituo  cha   Afya cha  ELCT  Ndolage  kilichopo   Bukoba lakini  alifia njiani.
Alisema baada ya gari lake kupekuliwa  kulikutwa na vilevi mbalimbali  ikiwemo Whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa.
Alisema jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia, Bi. Jackline kwa ajili ya kusaidia upelelezi na kuwa chanzo cha kifo hicho hakijajulikana