Saturday, May 17, 2014

Sifa 30 za mwanamke bora wa kuishi naye

Mwanamke ni mama mwenye nguvu unajua kwa nini? Sababu mwanamke alitoka katika ubavu wa mwanaume baada ya Mungu kufanya yafuatayo kwa mwanaume
A. Alimpa usingizi mwanaume
B. Alimfanyia upasuaji
C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mwanaume
D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume
E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume
F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke napenda ujue kuwa Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume amebeba vidonda kwa ajili ya mwanamke
Mwanamke ni mfupa mwanaume ni udongo hivyo mwanamke ni:
1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume – Bwana akisema ‘’nimefanya jambo jipya duniani mwamke atamlinda mwanaume
8. Chanzo cha baraka ya familia ( nitabariki Uzao wa tumbo lako)
9. Adui wa maadui wa familia (Uzao wa mwanamke utamponda kichwa nyoka na uzao wa nyoka (shetani ) utamponda kisigino (mwanzo)
10. Sauti ya familia (Bwana akamwambia Ibrahimu msikilize mkeo (mwanzo
11. Mponyaji wa familia yake na taifa
12. Mlezi wa huduma (wakamtumikia Yesu kwa mali zao(Luka8.3-4)
13. Mkombozi wa familia na taifa (kupitia mariamu mkombozi Yesu kristo alizaliwa (Luka i.29-35
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye (mwanzo 2:18)
15. Mwombezi wa familia,huduma na taifa (Tuwapate wapi wa mama waombolezaji
16. Mficha siri wa Mungu (Rebbeca alificha ni nani atayekuwa mtawala kati ya watoto wake wawili Esau na Yakobo.Baada ya kujua umuhimu wa mwanamke tunatakiwa kuangalia kiundani sana tabia 30 za mwanamke bora sio bora mwanamke tumeumia sana baada ya kuowa watu wasio sahihi katika eneo lilosahihi mwanamke bora ni mwamuzi wa familia ndio mleta mabadiliko katika familia mwanamke anayejua kwanini nipo hapa na ninafanya nini?
Mimi nimefanya utafiki kutokana na vitabu na maisha yanayotuzunguka nimeweza kugundua tabia 30 za Mwanamke anayeweza kunifaa mimi na wewe rafiki yangu tuziangalie kwa makini sana na kwa utafiki wa ndani:-
1. Moyo wa Mwanaume humwamini:
Moyo wa M wanaume humwanini Mwanamke bora sio bora Mwanamke, Mwanamke bora hujitahidi sana ili aweze kuaminika kwa mume wake maana Imani ni kitu muhimu sana katika mahusiano, mahusiano yakipoteza Imani hapo hakuna mahusiano, Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kujiaminisha kwa Mwanaume kuwa yeye ni mtu sahihi na chaguo sahihi kwa Mwanaume wake. Moyo ndio unaothibitisha kuwa huyu ni mtu sahihi au sio sahihi
Moyo ndio unamkubari mtu
Moyo ndio sauti ya mwisho
Moyo ndio chanzo cha upendo
Moyo ndio jibu la maisha yako ya mapendo
Moyo ndio chemichemi ya mapenzi
Moyo ndio unaoamini na kinywa husema yaliyo maamuzi ya moyo.
Huyu Mwanamke anatakiwa awe na jibu kwa Mwanaume- Upendo wa kweli hautambuliki kwa muonekano wa mtu bali upendo huambulika toka moyoni:- Hivyo Mwanamke bora ni Yule anayeweza kuushika moyo wa Mwanaume na kujiaminisha kwake.
2. Huondoa umaskini
Mwanamke bora katika maisha yako ni Yule mwenye mawazo mazuri ya kuondoa umaskini katika maisha yako- hana wazo baya, wengi wao wanatamani kuolewa ili awe na sifa mtaani kuwa ameolewa lakini ni tegemezi, hana wazo jipya la kubadilisha maisha yako. Hawa sio wanawake sahihi mawazo yake yanamtegemea mwanaume, wazo lake ni kuzaa watoto hana wazo la maendeleo, hajui maumivu ya maisha huwa wanarudisha nyuma ndoto zako kutokutimia kwa wakati wake. Mwanamke bora ni Yule mwenye mawazo ya maendeleo, mwenye hasira na umaskini mpenda mafanikio huyo ndiyo anafaa kuolewa
3. Kamwe hamtendei Mume wake mabaya
Mwanamke bora yaani niniamaanisha aliye sahihi ni Yule mwenye moyo safi kwa mume wake,
1. Hawazi mabaya bali mema kwa mume wake,
2. Hawezi kumtendea mume wake mabaya,
3. Hawezi kumuumiza mume wake,
4. Hawezi kumtonesha vidonda mume wake,
5. Hawezi kuumsaliti mume wake,
6. Hawezi kumtendea yasiyo haki mume wake,
7. Hawezi kumchafua mume wake na kumdharirirsha katika jamiii iliyowazunguka,
8. Hawezikumtukana Mume wake,
9. Hawezi kushabikia maumivu na mateso ya Mume wake,
10. Hawezi kuwa radhi na maadui wa Mume wake,
11. Hawezi kuwa jeuri kwa Mume wake,
12. Hawezi kumtendea Mume wake mabaya.
13. Amejaa heshima kwa Mume wake,
14. Adabu,
15. Utu wema anatunza uthamani wa Mume wake
16. Amejaa utiifu na upole kwa Mume wake
17. Amejaa unyenyekevu na uaminifu kwa Mume wake,
18. Amejaa amani na furaha ya kweli kwa Mume wake-
19. Anayeshinda uovu kwa wema,
20. Mwenye upendo wa kweli kwa mume wake. Huyu ndiye Mwanamke unayeweza kumuowa au kuishi naye na ndio sifa ya Mwanamke anayehitajika katika maisha yako. Mwanamke huyu ataheshimika na kuthaminiwa na watu na hatakosa upendo wa dhati kutoka kwa Mume wake.
4. Hufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii
Mke bora sio bora Mke ni mchapa kazi ni mtafutaji kwa mikono yake mwenyewe ni mjasiliamali hataki kuwa mzigo wa familia, kwa mikono yake anajenga, kwa mikono yake anasomesha watoto wake, kwa mikono yake anatunza familia yake kwa mikono yake anaheshimisha familia, mfanya kazi kwa bidii asiyechoka usiku na mchana sio mvivu, kwa mikono yake anafanya hategemei fedha za Mume wake- huyu anafaa kuwa Mke sahihi katika maisha sio mlinda mlango ni mtafutaji anakufaa sana katika maisha, napenda kukwambia mapenzi sio kuzaa, mapenzi kama pesa hakuna hutaona udhamani ni wake pesa ni jawabu la kila kitu sasa Mwanamke anajishughulisha anafaa sana katika maisha yetu ya leo- mapenzi ni kusaidiana.
Mwanamke sahihi hi Yule anayefanya kazi kwa mikono yake kwa bidii, Mwanamke ningependa kukushauri kuwa mali za Mwanammme ni mali za watoto na mali ya Mwanaume ni mali ya watu wengi, leo wanawake wengi wanateseka sana baada ya waume zao kufa wamenyang’anywa mali zao na ndugu wa kiume wanateseka sana kwa sababu walikuwa tegemezi kwa waume zao, Mwanamke wa kweli ni Yule mtafutaji na kuwawekea watoto zake mazingira mazuri ya maisha yao ya kesho.
5. Yeye ni kama meli ya biashara.
Mwanamke anafananishwa na meli ya biashara kwa sababu meli ya biashara inachukua bidhaa mbali mbali ndani yake, Mwanamke amebeba majukumu mengi sana katika maisha yake, mwanamke huyu ni:-
a) Mlinzi wa Mume wake.
b) Mzazi, mlezi mwenye watoto.
c) Mwangalizi mkuu wa familia yake na mazingira yake
d) Mwalimu Mkuu wa familia yake
e) Adui wa maadui wa familia yake.
f) Muombaji wa familia yake.
g) Kisima cha amani katika familia na ndugu wanaomzunguka.
h) Chanzo cha Baraka ya familia
i) Mficha siri ya familia- najua unajua kuwa Mwanamke ndio mficha siri wa familia anajua yote yanayofanyika ndani. Mwanamke ana majukumu mengi sana huku mtoto analia, baba naye anamwita huku watoto wanataka kusoma, wakwe wanataka chakula na mavazi huyu anatakiwa kusaidiwa lakini Mwanamke wa namna hii ndiye anayetakiwa katika maisha yako ndiyo maana amefananishwa na meli ya biashara malalamiko amepewa yeye matusi yeye, sifa njema yeye Mwanamke ni gari la familia. Nyumba yenye heshima inamuhitaji Mwanamke sahihi.
6. Huleta chakula chake toka mbali,
Mwanamke bora hategemei kulishwa na Mwanaume anasifa yakutafuta chakula chake toka mbali, hulisha familia yake kwa pesa yake, anahakikisha kuna kila kitu kinachohitajika katika famila yake, tegemeo la Mume wake Mume humwamini, nguzo ya familia yake, huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu, huyu anafaa ni chaguo lililo sahihi katika maisha yako.
7. Huamka kabla ya mapambazuko.
Mke bora huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kupanga mambo yake ataamka na kufanya usafi ndani, mazingira yake kiujumla huandaa chakula mapema hupangilia kazi kwa waliomo ndani mwake hufanya hivi na wewe fanya hivi sio Mwanamke anayeamka saa tatu (3) asubuhi au saa nne (4) asubuhi huyo ni mvivu hafai kuitwa Mwanamke bora bali ni bora Mwanamke hafai hana faida katika kuchangia maendeleo maana hata maandiko matakatifu yanasema “Siku njema huonekena alfajiri” mafanikio, Baraka, amaendeleo, huanza asubuhi Mwanamke anyefaa utamwona anaamka asubuhi sana na kupangilia mambo yake sawa, watu wa nyumbani watakula muda sahihi, wataenda shule wakiwa wamejaa amani mwenye maneno mazuri juu ya watoto wake na familia yake kwa ujumla. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa katika maisha yako, sio wanaoamka muda wanaopenda, Mwanaume anaandaliwa chai na mfanyakazi wa ndani, nguo za mume wako zinanyooshwa na mfanyakazi, maji ya kuoga mume wako yanaandaliwa na mfanyakazi wa ndani wewe sio Mwanamke sahihi na hufai kuitwa Mke bora wewe ni bora mke.
8. Hufikiri kununua shamba kisha hulinunua.
Mwenamke bora katika maisha hana mtazamo wa kununuliwa shamba, gari, nyumba na chochote cha maendeleo yake na familia hufanya mwenyewe akipenda kitu hununua hanunuliwi huyu ndiye Mwanamke wa Biblia mbunifu wa maisha anayetazama mbali sana kwa fedha yake hufanya maendeleo makubwa sana katika maisha yake, huyu ndiye Mwanamke bora anayefaa katika maisha yetu ndiyo Mwanamke anayetafutiwa na watu wenye maendeleo. Anaishi Kwa Jasho Lake, anategemea jasho Lake Hulima, hufanya kazi ili awezekutimiza ndoto zake.
9. Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
Mwanamke bora huwa tayari kufanyakazi kwa nguvu sana kwa ajili ya familia yake, anajituma kwa bidii kwa kila shughuri anayoifanya, ni mama mwangaikaji, mwenye kiu ya kutimiliza ndoto yake, mwenye kutambua wajibu wake kitaifa na kifamilia, mwenye mtazamo wa mbali, mwenye kiu na maendeleo, mwenye mzigo na familia yake, adui wa umaskini, ujinga na maradhi, mwenye kujituma kabla ya kutumwa. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa kuwa nayo katika maisha yake, huyu ndiye mama wa kibiblia sio bora Mke ni Mke bora.
10. Mwenye kuthamini shughuri zake.
Mwanamke bora anathamini sana shughuri zake kuwa zinafaida anaikubali kazi anayoifanya kuwa inafaa, hana tama na kazi za wengine ana heshimu kazi yake sana, hatishwi na maendeleo ya wengine maana naye ni Mwanamke anayejiamini sana kuwa hata yeye atafika, mwenye matumaini na Imani kubwa kwa kile anachofanya. Huyu ndiye Mke anayefaa katika maisha hutasikia malalamiko, hayupo katika mashindano, hana tamaa mbaya ningependa kukushauri kuwa mwanamke anayekufaa sio Mwanamke akiona mwenzake amevaa nguo Fulani naye anataka huyo hakufai ni muharibifu wa maendeleo atakurudisha nyuma kimaendeleo, tafuta Mwanamke huyo hapo juu.
11. Hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
Mwanamke huyu mjasiliamali hata usiku hufanya mambo yake kwa ajili ya maendeleo, hukanda unga wa maandazi, hushona nguo, vitambaa, hupanga mambo yake kabla ya siku mpya, wenye kutambua wakati alionao, huyu ndiye Mwanamke anaye kufaa katika maisha yako na ni Mwanamke wa kibiblia.
12. Asiye mchoyo.
Mwanamke bora sio mchoyo hufungua mikono yake kwa wahitaji, Mwanamke mchoyo hakufai maana ananyima Baraka katika maisha yako, Mwanamke mchoyo ni mchawi wa maendeleo, Mwanamke bora ni mtoaji, mwenye huruma na wahitaji ni mlezi wa wengi, kioo cha fmailia mwenye roho ya msamaha, ni mama wa wote walio wake na wasio wake, kwa aliyembariki na aliyemlaani, hana ubaguzi, mwenye moyo wa mama wa kweli, mwangalizi wa wote. Huyu ndiye mwanamke unaye muhitaji katika familia yako- usifanye makosa huyu ndiyo Mwanamke wa kibiblia.
13. Hana hofu na maisha ya watoto wake.
Mwanamke bora huwa anahakikisha kuwa anawaandalia watoto wake maisha mazuri, anawapeleka shule, msimamizi wa maendeleo yao, mtetezi wa haki zao, anahakikisha watoto wake wanakuwa na nguo, elimu nzuri, afya nzuri, kazi nzuri na anawaandalia maisha mazuri watoto wake hivyo anauhakika na maisha yajayo ya watoto wake. Huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu.
14. Mwenye kujipenda
Mwanamke bora anajipenda sana, anajidhamini, ni mzuri sana, mwenye kujikubali mwenyewe, adui wa uchafu, hawezi huwezi kumkuta mchafu hata watoto wake wanaoga, anapiga mswaki, anapika mafuta yake mazuri, na anaweka na marashi mwilini ili anukie vizuri sana, anatamanika, mavazi yake mazuri sana, anamvuto aonekanapo wakati wowote nyumbani na nje ya nyumba yake, Ua la familia, huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anamvuto wa kuwanaye karibu, kutembea naye anayethanini usafi wa mwili wake kuanzia chumbani kwake hadi nje huyu ndiye Mw anamke ninayekushauri uwe naye, huyu ndiye Mwanamke wa kibiblia.
15. Mume wake hujulikana malangoni.
Mwanamke bora humtambulisha Mume wake malangoni, Mwanamke ni pazia ya nyumba,
1. Pazia husitiri mambo ya ndani,
2. Pazia hupendezesha nyumba,
3. Pazia mlinzi wa nyumba,
4. Pazia huthaminisha nyumba,
5. Pazia hutambulisha wakaao ndani ya nyumba,
6. Mwanamke ni pazia ya Mume,
7. Ndiye anayempendezesha Mume,
8. Mlinzi wa Mume
9. Ndiye anaye mthaminisha Mume,
10. Andiye anaye mtambulisha Mume,
11. Kioo cha Mume
12. Mwanamke ni pambola Mwanaume, kama nyumba ikikosa pazia ni rahisi maadui kutambua vilivyomo ndani na kuvamia, ikikosa pazia hukaribisha maadui, Mwanamke ni pazia la nyumba ndiyo anayemtambulisha Mwanaume hata kama huyo Mwanaume ni mjinga Mwanmke anauwezo mkubwa wa kumuheshimisha Mwanaume mbele za watu, Mwanamke ndio mlinzi wa Mwanaume. Mwanamke anayejua wajibu wake hawezi kuibiwa Mume hata siku moja
“Sifa ya Mwanaume ni Mwanamke aliye naye”.
16. Mbunifu
Mwanamke bora nimbunifu wa maisha, hayuko nyuma huweza kufanya kitu na hufanya, mbunifu wa biashara, mitindo ya mavazi, hubuni na kuwauzisha wafanyabiashara, ni mtundu wa maendeleo, mwenye wazo jipy huyu ndiye Mwanamke anayehitajika.
17. Mwenye nguvu na kuheshimika
Mwanamke bora ana nguvu za maendeleo mwenye mali inayopatikana katika mikono yake mwenyewe na mwenye kuheshimika jamii inameshimu kwa maendeleo yake, inamthamini, inamuogopa, ni kioo cha wa mama wengine katika jamii inayomzinguka, mke bora anaheshimika na watu, ukiona unadaraulika unatakiwa kubadilika maana Mke mwema ana nguvu katika jamii na anaheshimika huyu huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha ya leo.
18. Hucheka afikiriapo wakati ujao (Future)
Mwanamke bora hana hofu na wakati ujao maana amekweisha udhibiti wakati ujao, Mwamnamke bora hutawala kesho hata kama hajaingia, hutawala jioni wakati ni asubuhi hivyo hana hofu na mambo ya kesho, Mwanamke bora anaucheka umaskini, magonjwa na ujinga huandaa mambo yake kwa wakati aliopo na kwa wakati ujao, huyu ndio Mwanamke anayetakiwa asiyekuwa na wasiwasi na kesho.
19. Hufungua kinywa Kunena kwa hekima.
Mwanamke bora amejaa hekima kinyuani SOPHIA - hekima ni kiongozi mzuri sana katika maisha, ni mlinzi, hekima ni mtawala, hekima ni utajiri, hekima ni heshima,
1. Mwanamke mwenye hekima hashindwi kuuitawala nyumba yake.
2. Mwanamke mwenye hekima hatishwi na watu na maneno yao.
3. Mwanamke mwenye hekima ni malkia wa nyumba yake,
4. Mwanamke mwenye hekima ni mkombozi wa familia yake.
5. Mwanamke mwenye hekima ni muamuzi wa haki katika familia yake,
6. Mwanamke mwenye hekima ni mdhibiti wa maovu katika famila yake.
7. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa famila,
8. Mwanamke mwenye hekima huondoa hasira kwa Mume wake.
9. Mwanamke mwenye hekima ni wa kujivunia,
10. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa ndoa yake/ huyu ndiyeMwanamke anaye tafutwa katika maisha yetu rafiki wa wote huyu ndiye Mwanamke anayehitajika katika maisha.
20. Huwashauri wengi kwa wema.
Mwanamke bora ni mshauri mzuri kwa wengine, mwenye kushauri mema wala sio mabaya kwa watu waliomzunguka yaani ni mponyaji wa familia za watu wengi hata taifa, ushauri wake hauna madhara kwa watu, kimbilio la wengi, sio mwenye mwenye kuharibu ndoa za watu, mchonganishi, mshirikina, muongo hapana, Mwanamke anatakiwa kutoa ushauri mzuri kwa wengi huyu ndiye Mwanamke tunayemuhitaji wengi.
21. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake.
Mwanamke bora anakuwa makini sana na kila kitu kinachoendelea au kutendeka katika nyumba yake anakuwa mwangalifu sana mna mambo ya nyumbani kwake kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yke, anatakiwa awe na muda wa kutosha na nyumba yake, hapendi ujinga nyumbani mwake, mahali pa kuonya anaonya, mahali pa kufundisha nafundisha, yeye ndiye mratibu mkuu wa yote yanayotendeka nyumbani, yeye ndiye kiongozi wa nyumba yake, mtendaji mkuu wa nyumba yake ndiye mjenzi wa familia bora hivyo Mwanamke kama huyu anyejua mjukumu yake ndiye anayetakiwa katika maisha yetu, sio kila Mwanamke umuonaye anafaa.
22. Kamwe hakai bure hata kidogo
Mke bora hakai bure lazima atakuwa na kitu cha kufanya, huwezi kumkuta kwenye vikao vya umbea, anazunguka zunguka kwenye nyumba za watu, maana ana mambo ya kufanya hakai bure hata kidogo ni mchapa kazi, anajituma, mbunifu wa mambo, anautaratibu wa maisha yake. Mwanamke ambaye yupo yupo tu huyo hatufai,ni chanzo cha matatizo, umbea, muongo, tafuta Mwanamke anayechapa kazi yuko (busy) na shughuri za kifamilia, kiofisi mwenye maendeleo huyo ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha.
23. Watoto wake huamka na kumshukuru.
Mke bora watoto wake wanafuraha naye, wanamshukuru sana mama yao, maana amewajengea maisha mazuri amewafundisha mambo mazuri, amewalea vizuri, watamuheshimu sana mama yao na kumpenda, watamlinda na kumtunza mama , mama wa kweli husifiwa na watoto wake, watoto wanajisikia amani wanapokuwa naye, mwenye maadili mema mbele ya watoto wake,. Mfano wa kuigwa kwa mambo mazuri anayowatendea watoto wake hivyo shukurani hazitaweza kundoka midomoni mwa watoto wake huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa.
24.Mume huimba sifa zake
Mke bora Mume wake humsifia kwa sifa njema Mume hutangaza uzuri wa Mke wake, hutangaza mtendo mazuri ya Mke wake, hujivunia na anajisikia bahati kuwa na mke kama huyo, mwenye tabia njema, mtiifu, mpole katika maisha yake mwenye kujiheshimu, anyempenda mume wake na watoto zake, msema kweli, mlinzi mwaminifu, Mwanamke mwenye maendeleo huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu aliyekubarika katika moyo wa Mume wake mpenzi.
24. Mwenye kumcha Mungu
Mke bora ni Yule mcha mungu anayempenda Mungu mtu wa Ibada mwenye hofu ya Mungu anayeichukia dhambi, mpenda maombi na Neno la Mungu huyu ndiye Mke sahihi katika maisha, mwenye mzigo wa maombi kwa ajili ya Mume wake na watoto wake na wote waliomzunguka huyo ndiye chemichemi ya mabadiliko ya familia, mleta ukombozi wa fmailia huyu ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha yetu ya leo.
25. Mwenye kupenda elimu.
Mke bora ni Yule anyependa Elimu. Elimu imegawanyika katika sehemu mbili. Kuna Elimu inayopatikani mashuleni na Elimu inaopatikana katika mazingira unayoishi, wazazi na jamii iliyokuzunguka Mke bora anapenda kujifunza mazuri kwa wengine, mafanikio yao, sio mjuaji, yupo tayari kurekebishwa na kubadilika, anayekubari kushauriwa huyo ndiye Mwanamke anayefaa maana ni msikivu na mpenda mabadiliko yenye faida
26. Huandaa chakula kwa familia yake.
Mke bora ni mpishi mzuri wa chakula katika familia yake hategemei wafanyakazi yeye ni Mwalimu wa wengine mume humsifia Mkwa kwa mapishi yake mazuri nay a usafi wa hali ya juu sana . mpendwa najua unajua kuwa kuna baadhi ya wake za watu hawajui kupika, sio mbunifu wa mapishi mchafu katika maandalizi yake huwa ni wake wasio bora, wanavunja nyumba zao, tafuta Mke ambaye hana chakula cha kukariri bali bali ni mbunifu wa mapishi ni msafi anayejipenda mwalimu wa mapishi huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu ya leo.
27. Mwenye sifa njema.
Mke mwema anasifa njema katika jamii iliyomzunguka hana tabia za uzinzi na uasherati, hana tabia ya ulevi na matusi, hana tabia ya umbea na uchonganishaji, hana tabia ya kiburi na jeuri Mke mwema ni rafiki wa watu wengi amejaa shukrani na hana mawazo mabaya Mke bora hutambulika na matendo yake katikajamii inayomzunguka.
28. Mwenye kudhamini na kutunza upendo.
Mke bora anajua maana ya upendo na gharama zake, anajua maumivu na vidonda vya mapenzi, anajua nguvu ya upendondani ya mtu, anatambua hisia kali ya upendo, Mwanamke wa namna hiyo hataweza kukusaliti, atakuheshimu na kukupenda kweli kutoka moyoni mwake hatagawa upendo wakko kwa wengine, atalinda penzi lake kwa ajili yako, anaheshimu mwili wake huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anayejua kwanini umempenda yeye na umewaacha wengine mwenye tabia njema. Huyu ndiye Mama wa familia bora sio bora familia.
29. Mwenye wivu wa maendeleo
Mke bora ana wivu wa maendeleo hana wivu wa kijinga unaoweza kusababisha amani katika ndoa kuondoka .Mwanamke ni mponyaji wa ndoa yake ni kweli Mwanamke anatakiwa awe na wivu kwa Mume wake lakini vilevile lazima awe na Imani na Mume wake, kuna wivu unaoweza kuharibu amani ya nyumba lakini kuna wivu unaoweza kujenga nyumba. Inategemea Mama ana wivu wa namna gani sio wote walio karibu na Mume wako, wako katika mahusiano na Mume wako, Mwanamke bora hufanya utafiti wa jambo na kuwa na uhakika naolo na huliwasilisha kwa hekima sana. Wivu ni mzuri ukitumiwa vizuri na pendo la kweli lina wivu lakini uwe wa maendeleo katika maisha yenu.
Mpendea wangu huo ndio utafiti wangu kuhusu mwanamke anayefaa katika maisha yako nimetumia kitabu cha (Mithali 31:10-31) (Goodnews bible)
Kumpata Mwanamke bora sio kitu rahisi lakini kupitia mafundisho ya vitabu kama hivi, vitafungua ufahamu wako mkubwa na kumtafuta Mke sahihi kimungu- kibiblia.

No comments:

Post a Comment