Na Theonestina Juma, Kagera
WANAFUNZI wawili wa shule ya
sekondari Kamuli Wilayani Kyerwa, wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya
kupigwa na radi usiku wakiwa wamelala.
Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana mjini Bukoba na kuthibitishwa na Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Bw.Marco
Renatus tukio hilo limetokea usiku wa kuamukia Agosti
18, mwaka huu.
Wanafunzi waliofariki dunia wametajwa
kuwa ni pamoja na Amon Anaseth mwanafunzi wa kidato cha nne pamona na Onesmo
Odilo mwanafunzi wa Kidato cha kwanza katika shule hiyo ya Kamuli.
Aidha aliyejeruhiwa katika
tukio hilo ametajwa kuwa ni Filbert Jacksonary ambaye amepatiwa matibabu katika
kituo cha afya kilicho wilayani humo na hali yake inaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa Makamu wa shule
hito, Bw. Marco wakati radi ikipiga wanafunzi
hao walikuwa ndani wamelala.
Alisema radi hiyo imebomoa
ukuta wa chumba cha kwanza na cha pili walimokuwa wamelala wanafunzi hao.
Hili ni tukio la pili ndani ya
wiki moja ya radi kupiga na kuwauawa raia mkoani hapa katika wilaya ya Karagwe
kata ya Kanoni.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment