Wednesday, October 2, 2013

Majambazi 88 wanaswa miongoni mwao watano ni walanguzi wa silaha na wasambazajia



Na Theonestina Juma, Bukoba
OPERESHENI kimbunga awamu ya pili inayoendelea katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa imefanikiwa kuwanasa majambazi 88,miongoni mwao watano  wamebainika kujishughulisha na biasharaya kulanguzi wa silaha kutoka katika mnada wa nchi jirani kwa sh. 300,000 na kuingiza nchini na  kuuza kwa mamilioni ya fedha.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Kamishina wa Operesheni Kimbunga, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari  mjini Bukoba juu ya maendeleo ya opereheni hiyo inavyoendelea hadi hivi sasa.
Kamanda Sirro alisema jumla ya majambazi 88 wamekamatwa katika zoezi hilo miongoni mwao watano ni wanaojihusisha na biashara ya kwenda nchini jirani ya Burundi kulangua silaha hizo kwa sh.300,000 na kuingiza nchini na kuziuza kuanzia sh. milioni 1.5 na kuendelea kwa bunduki aina ya SMG.
Halikadhalika miongoni mwa hao watano watatu wamebainika kujihusisha katika usambazaji wa silaha hizo kwa wateja humu nchini ambapo majambazi hao wote wamebainika kuwa ni Watanzania.
“Kuna jambazi mmoja ambaye ni Raia wa Tanzania yeye awali alikuwa akifanya biashara ya kuuza mbuzi nchini Burundi baada ya kuwalangua kutoka humu nchini, lakini baadaye alishawishia na watu wengine kuwa biashara ya mbuzi halilipi bali biashara ya kuuza silaha ndiyo inalipa naye akajiunga katika shughuli hiyo”alisema Kamanda Sirro bila kuwataja majina yao.
Alisema katika operesheni hiyo, awamu ya pili ilioanza Septemba 21 hadi Oktoba mosi mwaka huu, wamefanikiwa kuwakamata  wahalifu 529 wahamiaji haramu  wakiwa ni 425 kutoka katika mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera.
Alisema wahamiaji haramu waliorushwa kwa  maamuzi ya mahakama ni 159, waliorudishwa kwa hiari ni 122, walioachiwa huru 39 huku wanaoendelea kuhojiwa wakiwa ni 105.
Alisema kati ya wahamiaji haramu hao waliokamatwa, Wanyarwanda  ni149, Warundi180, Kongo 14, Waganda 82,
Pia watu watano wanashikiliwa kwa tuhuma ya kutorosha na kuwahifadhi wahamiaji haramu   pamoja na majamngili 11.
Halikadhalika silaha mbali mbali zipatazo 23 zimekamatwa ambazo ni pamoja na SMG 3,pistol 2, magobole 18, risasi 484 za bunduki aina ya SMG/SAR  zikiwa ni 471 na pistol 13, magazine  mbili na bomu la kutupwa kwa mokono likiwa ni moja na sare moja ya jeshi la nchi jirani ya Burundi.
Katika hatua nyingine Kamanda Sirro alisema ng’ombe 2,220 wamekamatwa ambapo ng’ombe  103 mali ya Bw. Kalemela  George wilayani Biharamulo imeamuriwa na mahakama kutaifishwa  baada ya kuwangiza katika hifadhi ya taifa  Biharamulo  kinyume cha sheria na hivyo kutoa wito kwa wanaofanya biashara ya nyama mkoani Kagera kwenda  kununua kwa ajili ya kuchinja na kuuza.
“Hatua hii ya kutaifishwa na serikali hao ng’ombe itakuwa na matokeo katika jamii, hivyo wale wanaouza nyama mabuchani wanaohangaika kutafuta ng’ombe wa kuchinja kwa ajili ya kupata nyama ya kuuza wasisite kwenda wilayani Biharamulo kununua ng’ombe”alisema.
Alisema ng’ombe wanaobaki bado wanafanya utaratibu wa kufikisha kesi zake mahakamani ili nao waweze kutaifishwa.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Missenyi, Kanali Issa Njiku akizungumzia juu ya zoezi hilo alisema zoezi hilo bado linaendelea na ni endelevu na kwamba linaenda kiawamu  na hivyo wanaodhani kuwa zoezi hilo limekwisha wanajidanganya.
Alisema ni wajibu wa wanannchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa maofisa wanaofanya kazi ya kuwatafuta majangili, majambazi, wahamiaji haramu kutoa ushirikiano kwao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment