Na Theonestina Juma, Bukoba
MADIWANI sita kati ya tisa waliokuwa
wanashtakiwa kwa kosa la kushindwa kududhuria vikao vya vya Halmashauri ya
Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamevuliwa vyadhifa zao na Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mkoa wa Kagera.
Akisoma hukumu hiyo leo mbele ya
Mahakama hiyo,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Uiso, alisema madiwani
hao wanavuliwa udiwani huo kutokana na mahakama hiyo kuidhika na ushahidi wa
pande ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa madiwani
hao,walikuwa wakikataa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani pamoja na vikao
mbali mbali vya baraza hilo jambo lilisababisha kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa manispaa ya Bukoba.
Uiso amesema kuwa ushahidi wote
uliotolewa mahakamani hapo umeweza kuridhisha mahakama bila kuwa na shaka
lolote.
Madiwani waliovuliwa nafasi zao za
udiwani ni pamoja na Bw. Samuel Ruangisa kata Kitendaguro(CCM) Bw.,Deusdedith
Mutakyahwa kata Nyanga(CCM,),Bw.Yusuph Ngaiza kata Kashai(CCM),Bw.Dauda
Kalumuna kata Ijuganyondo (CC) , Bi. Murungi Kichwabuta Viti maalumu(CCM)na
Rabia Badru viti maalumu (CUF).
Hata hivyo, mahakama hiyo imetupilia
mbali malalamiko dhidi ya madiwani wengine wawili Bw. Richard Mwemezi kata
Miembeni(CCM)na Bw.Israel Mlaki kata Kibeta(CHADEMA) kwa madai kuwa hawa hawahusiki moja ka moja na malamiko hayo
kwani na kwa Bw.Richard kuwa hakuwa
mjumbe wa kamati hiyo na Israel Mraki aliweza kuhudhuria baadhi ya vikao hivyo.
Kutokana na hali hiyo Mahakama imewaamuru madiwani hao saba waliovuliwa udiwani kulipa gharama za uendeshaji wa kesi
hiyo kwa mlalamikaji.
Hukumu ya kesi hiyo iliyotumia takribani
masaa mawili, ilivuta hisia za watu na kuwafanya wagawanyike katika pande mbili
zilizowahusu wafuasi wa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Hamis Kagasheki(CCM) na
aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyoDkt. Anatory Amani,ambavyo mvutano wa makundi hayo
yalianza kuibuka mara tu baada ya kuwepo malumbano dhidi ya vigogo hao wa
kisiasa.
kesi hiyo ilifunguliwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Afya, elimu na uchumi Bw.Chief Kalumuna, ambaye pia ni diwani wa kata
Kahororo(CCM) ambapo madiwani hao ambao
walikuwa wajumbe wa kamati yake walikaidi kuhudhuria vikao zaidi ya tano.
Alitaja baadhi ya vikao walivyotakiwa
kukaa na tarehe kuwa ni pamoja na Julai 19, Agosti 1,septemba 23,novemba 11 na
novemba 14 mwaka 2013.